Kukausha njia kutoka athari za mvua
Question
Ni nini malipo ya kuzikausha njia kutoka maji ya mvua?
Answer
Hakika kuzikausha njia kutoka maji ya mvua kwa kuyaondoa maji kwenye mahali mahsusi, ni aina ya kuondoa adha njiani, na ni miongoni mwa kazi njema zinazopendekewa katika sheria, ambapo kuondoa adha njiani mwa watu ni katika sifa za Imani, imesimuliwa na Abu Hurairah (R.A.) kwamba alisema: Mtume (S.A.W.) alisema: “Hakika Imani ni viwango sabini na kadhaa, kiwango cha juu zaidi chake ni kusema: Hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na cha chini zaidi ni kuondoa adha njiani, na haya kiwango cha imani” Imekubaliwa na wote. Kwa hiyo, anayefanya hivyo kwa kuondoa adha kwa kuzikausha njia kutoka maji ya mvua hustahili malipo mema duniani na Akhera; kwa mujibu wa hadithi iliyosimuliwa na Abu-Hurairah (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Nimemwona mtu aliyekuwa akifurahia peponi kivulini mwa mti alikuwa ameukata njiani mwa watu ili awaepusheni adha yake” na katika riwaya nyingine ya Imamu Bukhary katika kitabu chake cha Sahih alisema Mtume (S.A.W.): “Mtu mmoja alikuwa akitembea njiani akakuta tawi la mwiba akaliondoa, akashukuriwa na Mwenyezi Mungu na kusamehewa madhambi yake” Imesimuliwa na Muslim.