Kuhamisha na kupandikiza viungo

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhamisha na kupandikiza viungo

Question

Kuhamisha na kupandikiza viungo

Answer

Mustafa Abdulkereem

Mtafiti kitengo cha tafiti za Kisharia ofisi ya Mufti wa Misri

Utanguzi

Sharia ya Kiislamu imewekwa kwa hekima na masilahi ya waja katika maisha ya duniani na Akhera, imekuja ili kulinda roho za watu, akili zao, dini zao, heshima zao pamoja na mali zao. Mambo haya matano ndio makusudio makuu ya sharia, au mambo ya lazima kuyachunga katika dini zote.

Kulinda roho ni miongoni mwa makusudio makubwa na ya kwanza; Sharia imekataza mtu kujidhuru kwa hali yoyote, na imeamrisha kufuata njia za kujilinda yeye mwenyewe, uhai wake na usalama wake, na kuizuia na maudhi na madhara, na ikamuamrisha kujiepusha na yaliyoharamishwa na yenye kuaharibu na kuangamiza, na ikamuongoza kujitibu wakati wa maradhi kwa kufuata njia zote za matibabu.

Miongoni mwa njia za matibabu za kisasa ambazo zimeleta matokeo mazuri ya matibabu na zimefikia malengo haya ni “Kuhamisha na kupandikiza viungo vya Mwanadamu”.

Na makusudio ya viungi ni: Sehemu yeyote ya mwanadamu ikiwemo nyuzinyuzi, selli na damu.

Upasuaji wa kupandikiza viungo unaanza kwa kuchukuliwa kiungo kinachotaka kupandikizwa kutoka kwa mtu mwenye kiungo hicho kisha kukata kiungo mfano wake ikilazimu hilo ili kiungo kipya kichukue nafasi yake, kisha kukiweke kiungo kilichohamishwa katika sehemu yake iliyoandaliwa katika kiungo cha mtu anayehamishiwa.

Na tumerefusha maneno katika tafiti hii katika yale yanayohusiana na suala hili kwa upande wa Sharia. Na tumegawa katika Sura mbili:

Sura ya kwanza, ina kichwa: Tafiti ya kuhamisha viungo, na ina sehemu saba kama zifuatavyo:

Sehemu ya kwanza: Kumisha viungo kutoka katika mwili wa mwanadamu aliye hai kwenda sehemu nyingine katika mwili huohuo.

Sehemu ya pili: kuhamisha viungo kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili mwingine kama huo.

Sehemu ya tatu: kuhamisha viungo visivyo vya mtu mmoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili wa mwanadamu kibiashara.

Sehemu ya nne: kuhamisha viungo visivyo vya mtu mmoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili wa mwanadamu kwa kujitolea.

Sehemu ya tano: kuhamisha viungo vya mwanadamu kutoka katika mwili wa maiti na kuvipandikiza katika mwili wa mwanadamu aliyehai.

Sehemu ya sita: Hukumu ya kuhamisha na kupandikiza viungo vya uzazi.

Sehemu ya saba: Hukumu ya kuhamisha kiungo kutoka kwa mnyama kwenda kwa mwanadamu.

Na Sura ya pili: Ina anwani: Masuala yanayofungamana na unafiti huu, na ina sehemu nne kama ifuatavyo:

Sehemu ya kwanaza: Masuala katika hukumu ya kuhamisha damu. 

Sehemu ya pili: Masuala ya kuhamisha seli za shina.

Sehemu ya tatu: Masuala ya yanayofungamana na kufa kwa ubongo.

 Sehemu ya nne: Masuala katika hukumu za kurudisha viungo vilivyokatwa kwa hukumu ya Hadi au Kisasi.

Mwisho kuna matokeo muhimu ambayo tumeyafikia mwishoni mwa utafiti huu.

Katika tafiti hii tumetegemea vitabu vya Fiqhi vinavyotegemewa, pia tumetumia baadhi ya vitabu vya tafiti za kitabibu, na hasa kitabu cha “Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity Mwalimu Msikiti mtukufu wa Mtume, kitabu hiki ni Tasnifu ya PHD ya kitengo cha Fiqhi Chuo Kikuu Cha Kiislamu, Madina.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atufungulie ufunguzi wa wajuzi, na atuwafikishe kufikia makusudio ya kutuumba kwake, na aibariki tafiti hii na ilete manufaa, yeye ndiye mbora wa kuombwa na tegemeo bora

.

Sura ya kwanza

Tafiti za kuhamisha viungo

Sehemu ya kwanza: Kumisha viungo kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda sehemu nyingine katika mwili huohuo.

Sehemu ya pili: kuhamisha viungo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili mwingine kama huo.

Sehemu ya tatu: kuhamisha viungo visivyo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili wa mwanadamu kibiashara.

Sehemu ya nne: kuhamisha viungo visivyo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili wa mwanadamu kwa kujitolea.

Sehemu ya tano: kuhamisha viungo vya mwanadamu kutoka katika mwili wa maiti na kuvipandikiza katika mwili wa mwanadamu aliyehai.

Sehemu ya sita: hukumu ya kuhamisha na kupandikiza viungo vya uzazi.

Sehemu ya saba: Hukumu ya kuhamisha kiuongo kutoka kwa mnyama kwenda kwa mwanadamu.

Sehemu ya kwanza

Kuhamisha kiungo kutoka sehemu ya mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda sehemu nyingine katika mwili huohuo

Miongoni mwa njia za kuhamisha viungo ni kuhamisha kiuongo kutoka katika mwili wa mwanadamu kwenda sehemu ya nyingine ya mwili wake. 

Masilahi yanayopelekea suala hili ima ulazima, au haja au mapenzi ([1]).

Baadhi ya mifano ya masilahi yanayopeleka ulazima: Kama upasuaji wa moyo na mishipa ya damu, ambapo daktari huhitaji kutumia vena au mishipa ya damu ili kutibu kuziba au kuchanika mishipa, na kumuokoa mgonjwa aliyeziba au kuchanika mishipa kunakuwa kwa kupandikiza vena iliyochukuliwa kutoka katika mwili wa mgonjwa huyo huyo ([2]).

Mfano wa masilahi yanayopelekea kufikia ngazi ya mahitaji: Ni kama upasuaji wa ngozi kama itaungua kufikia mahitaji ya kitabibu, ambapo daktari anahitaji kuchukua sehemu salama katika ngozi ya mgonjwa na kuipandikiza sehemu uliyojeruhiwa.

Na mfano wa masilahi unaopeleka hilo ambao unafikia ngazi ya mapenzi: kama inavyokuwa katika operesheni ya kupandikiza nywele ambao unategemea kuhamisha nywele kutoka sehemu yenye nywele kwenda sehemu yenye kipara, ambapo huchukuliwa kipande cha ngozi nyuma ya kichwa, kisha kidonda hufungwa vizuri na athari yote huondoka, kisha kipande hiki hukatwa kuwa vinywele vidogodogo na huwekwa katika sindano malumu, na kupandikizwa eneo lenye kipara.

Na katika hali mbili za kwanza zinajuzu, kama matagemeo ya daktari yatakuwa ni ya mafanikio kwa asilimia kubwa katika upasuaji huu kuliko madhara yatakayopatikana.

Na hukumu ya kujuzu hali mbili hizi zimewekwa kwa njia ya kipimo cha usawa (Al-Qiyas); kwa sababu ikijuzu kukata kiungo na kuondolewa ili kuokoa nafsi na kuiondoshea madhara, basi kujuzu kuchukua sehemu katika kiungo hicho na kukihamisha sehemu nyingine ili kuiokoa nafsi au kuindoshea madhara ni bora zaidi.

Na njia ya hilo: kwamba asili kunajuzu kuondosha na kukata kiungo chote kwa kutafuta kuokoa nafsi na kuindoshea madhara, na tawi ni kuondosha sehemu ya kiuongo pamoja na kubakia sehemu iliyoondolewa katika sehemu nyingine, pamoja na hilo ni kwamba sehemu iliyoondolewa itarudi tena kama ilivyo katika kuchukua ngozi nzima ili kuipandikiza sehemu iliyoungua, hapa kunakuwa ni bora zaidi kuzingatiwa na hukumu ya kujuzu inatokana na asili.

Aina hii yaupasuaji wa kukata kiungo kinachohitajika kukatwa imejuzishwa kwa kauli za wanazuoni wa Fiqhi ([3]).

Ama hali ya tatu ya upasuaji wa kupenda, hukumu yake inatofautiana kwa kutofautiana aina yake, kama itakuwa ni kimahitaji, na masilahi yatakayopatikana yatakuwa makubwa kushinda madhara, na kukawa hakuna njia ya mchezo katika kufanyika kwake basi kauli ya kujuzu itakuwa ni sahihi, na Mwenyezi Mungu ndie anayejua zaidi.

Sehemu ya pili

Kuhamisha viungo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili wa mwanadumu mwingi aliyehai

Miongoni mwa njia za kuhamisha viungo, ni kuhamisha kiungo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda katika mwili mwingine wa mwanadamu aliyehai, na maana ya kiungo kimoja kimoja tunayoilenga hapa: Ni viungo ambavyo havina mbadala wakufanya kazi yake, kuvihamisha hasababisha kifo kwa mtu wake; kwa sababu mwili hauwezi kuishi bila ya kiungo hicho, ni kama moyo, ini lote kwa mfano, viungo hivi ni haramu kwa mwanadamu kuvitoa kwa mtu mwingine kuchukua kutoka kwa mtu mwingine, sawasawa iwe kwa njia ya biashara au kujitolea.

Vilevile ni haramu kwa daktari kusaidia kuvihamisha viungo hivi na kuvipandikiza; na hii kutokana na kusababisha kifo kwa mtu anayechukuliwa kiungo hichi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.” [Albaqara:195] na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni” [Annisaai:29] na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui” [Almaaida:2].

Aya kwanza imetoa dalili ya kuharamisha mtu kutumia kitu kitakachomuangamiza, Aya ya pili imetoa dalili ya kuharamisha mwanadamu kujiua mwenyewe, na kujitolea kiungo kimoja kimoja ambacho kitamsababishia kifo, kukawa ni haramu, ikiwa ni haramu imethibiti katika kujitolea, basi uharamu katika kuuza ni haramu zaidi; kuuza na kujitolea vinashirikiana katika umiliki na kuuza ni zaidi ya kujitolea kwa kuwepo thamani.

Ama Aya ya tatu, inachukua katika hii uharamu wa kushiriki daktari katika kufanya upasuaji wa kuhamisha kiungo na kukipandikiza; kwa sababu hapa anakuwa msaidizi katika maasi na madhambi, na kusaidia dhambi kumekatazwa kwa matini ya Aya.

Miongoni mwa kanuni za kisharia zilizopitishwa ni kwamba madhara hayaondolewi kwa madhara ([4]), hakujuzu kuondosha madhara kutoka kwa mtu mwenye kiungo kilichoharibika, kwa kuharibu kiungo cha mwanadamu mwingine, roho ya wa kwanza si bora kuilinda kuliko roho ya pili na maisha yake, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.

Sehemu ya tatu

Kuhamisha viungo visivyo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda mwili wa mwanadamu mwingine kibiashara

Miongoni mwa aina za uhamishaji viungo ni Kuhamisha viungo visivyo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda mwili wa mwanadamu mwingine kibiashara, viungo visivyo kimoja kimoja ni viungo ambavyo havina mbadala wakufanya kazi zake, na kuhamisha kwake hakusababishi kifo kwa kawaida, na hilo huwa  katika viungo vinavyofanana, kama figo, au vinavyorejea upya kama ngozi na damu.

Wala hakujuzu kwa mwanadamu aliyetukuzwa na Mola wale kuviuza au kuuza kiungo chochote katika mwili wake, na biashara hio ni batili.

Na dalili ya uharamu ni Hadithi iliyopokelewa na Bukhari kutoka kwa Abuu hurayra Allah amuwie radhi kwamba Mtume S.A.W. amesema: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “watu watatu nitawahoji siku ya Kiama: mtu aliyepewa amana kwa kuapa kwangu kisha akafanya khiana, mtu aliyemuuza mtu huru na akala thamani yake, na mtu aliyemuajiri mtumishi, akamfanyia kazi yake, na hakumpa ujira wake” ([5]).

Hadithi hii inatoa dalili ya kuharamisha kumuuza mtu huru –Ibnu Al-Mundhir amenukuu kwa makubaliono ya Wanazuoni waliowengi([6])- vilevile uharamu wa kuuza viungo vyake; ama kumuuza mtu huru uharamu wake umethibiti katika tamko la Hadithi, ama kuuza viungo vyake kwa sababu ya uharamu katika Hadithi ni uhuru, na kanuni ni kwamba kuitungika hukumu ya Hadithi kwa tawi kumeruhusiwa kwa sababu maalumu ikiwemo asili ya tawi, na kila sehemu ya mwanadamu huru inathibiti uhuru wake pia, kwa dalili kwamba mtumwa ambaye anamilkiwa na watu wawili mmoja wao akimuacha huru, mtumwa huyu anakuwa baadhi uhuru baadhi mtumwa, hii ikatoa dalili kwamba uhuru unaweza kuwa nusu na imethibitisha sehemu zote za mwaadamu. 

Ama biashara kuwa batili; kwa sababu mtu huru au viungo vyake si sehemu ya bishara, kwani miongoni mwa sharti za kusihi biashara- kwa makubaliano ya wanazuoni- kuwa kitu ambacho inafaa kuwa biashara, na hii kwa kuwa: mali inayothaminiwa, inayomilikiwa kunajuzu kunufaika nayo.

 Na mwanadamu sio mali yenye thamani, hivyo hakujuzu kumuuza wala kuuza kitu katika viungo vyake, na ufafanuzi wa hilo ni kwamba: Mali imeumbwa ili kutengenezea masilahi yetu, ama mwanadamu Mwenyezi Mungu amemuumba kuwa mmiliki wa mali, na kati ya kuwa kwake mali na kuwa kwake mmili wa mali kunapingana, kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika kauli yake: “Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi.” [ Al-Baqara:29].

Na miongoni yanayotolea ushahidi suala hili ni tanzu za Fiqhi, ni yale yaliyokuja katika Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa katika kauli yao ya uharamu wa kuuza maziwa ya mwanadamu wakitoa sababu ya kuwa si mali inayotiwa thamani ([7]), na Madhehebu ya Imamu Malik na Shafi na Hanbal wamejuzisha hilo ([8]). Lakini kipimo cha hilo ni kipimo pamoja na tofauti; kwa sababu maziwa yanarejea upya, na kuendelea kuwepo kwake katika matiti ya mwanamke huenda yakamdhuru, kinyume na viungo, ambavyo ndio uti wa mwili wa mwanadamu.

Mpingaji akipinga kauli yetu kuwa mwanadamu sio mali kwa sababu sharia inamlazimisha aliyefanya shambulizi kulipa fidia, na hii inatoa dalili kwamba mwili wa mwanadamu unathamani mali anaidhamini anayeuharibu, basi jibu lake ni: kwamba asili katika kudhamini katika Fiqhi ya Kiislamu ni mfanano kamili, na hilo ni kama katika kisasi, ama fidia si mfano wake; kwa sababu mfanano kati ya vitu viwili hujulikana kwa sura au maana, na kupasa fidia na kiapo ili kulinda nafsi isiangamie ([9]).

Rai nyingine

kuna rai nyingine katika suala hili; Baadhi ya wanazuoni wanasema kwamba kunajuzu kuuza viungo ([10]), na wametoa dalili katika hilo kwa mfano uliotangulia katika kipimo cha usawa (Al-Qiyas) kwa maziwa ya mwanadamu, na katika kumlazimisha fidia mwenye kumshambulia mtu, na mjadala wa hilo umeshatangulia, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.

Na pakisemwa: Je, kunajuzu kwa mwenyekujitolea baadhi ya viungo kuchukua pesa si kwa njia ya badala bali kwa kuhamisha umiliki [11] (RAF-UL-IKHTISAS) kama kulivyojuzishwa kufanya hivyo katika kuhamisha damu- kama itakavyokuja.

Tumesema kuwa: Damu ni kitu kinachorejea upya, sehemu iliyotolewa inakuja nyingine sehemu yake, na hili haliwi kwa kila kiungo; viungo vipo vinavyorejea upya seli zake, kama ini, sehemu yake iliyochukuliwa hujirejea upya seli zake mpya, na kuna viungo visivyojirejea seli zake kama figo.

Ama viungo ambavyo hujirejea seli zake, hivi kunajuzu kuchukua mali kwa kuhamisha umiliki (RAFUL-IKHTISAS); na hii kwa kuchukua sehemu tu katika kiungo si chote, ili ibakie sehemu itakayojirejea seli ambazo zimetolewa.

Ama viungo ambavyo havijirejei seli zake, hakujuzu kuchukua pesa kwa kuhamisha umiliki (RAFUL-IKHTISAS) ila kutakapokuwa na kiungo kinachofanya kazi ya kiungo husika, na mfano wa hilo ni: Kuwa mtu anayetoa kiungo chake ana figo mbili zinazofanya kazi vizuri, kunajuzu kwake kutoa moja kwa kuchukua fedha kwa njia ya kuondoa umiliki (RAFUL-IKHTISAS) itakapokuwa nyingine ipo na inafanya kazi vizuri, ama kama kitakuwa kiungo sio kinachojirejea upya na hakukuwa na kiungo kinachofanya kazi yake, basi hakujuzu kuchukua pesa kwa njia ya kukiuza au kuhamisha umili (RAFUL-IKHTISAS) wala njia yeyote; kwa kuwa hilo husababisha kifo kwa mtu anayechukuliwa kiungo chake, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.” [Albaqara:195] na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “ Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni” [Annisaai:29] na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui” [Almaaida:2].

Miongoni mwa kanuni za kisharia zilizothibiti ni kwamba madhara hayaondoshwi kwa madhara ([12]), hivyo basi hakujuzu kuondosha madhara kutoka kwa mtu mwenye kiungo kilichoharibika kwa kuharibu kiungo cha mwanadamu mwingine.

Sehemu ya Nne

Kuhamisha viungo visivyo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda mwili wa mwanadamu aliyehai kwa njia ya kujitolea

Miongoni mwa aina za kujitolea viungo ni kuhamisha viungo visivyo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda mwili wa mwanadamu mwingine kwa njia ya kujitolea, viungo visivyo kimoja kimoja tumevielezea katika sehemu iliyopita.

Kunajuzu kisharia kuhamisha na kupandikiza viungo visivyo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliyehai kwenda mwili wa mwanadamu mwingine kwa njia ya kujitolea pamoja na kuchunga vidhibiti vifuatavyo:

Kupatikana hali ya ulazima au haja ya kisharia ambayo kupandikiza kunakuwa ndio njia pekee ya matibabu ambayo inaamuliwa na madaktari.

Kukubali mwenye kuchukuliwa kiungo chake pamoja na kuwa amebaleghe mwenye akili na hiari.

Kuwa kuhamisha kiungo husika ni kwenye kuhakikisha masilahi yaliyothibitishwa kwa mwenye kuhamishiwa kwa mtazamo wa kidktari, na kitakachomzuia na madhara yaliyothibitishwa kama hatohamishiwa.

Kuhamisha kiungo kusisababishe madhara makubwa au madogo yanayothibitishwa kwa anayechukuliwa kiungo, kuleta athari mbaya katika hali yake au mali yake kwa njia inayothibitishwa kidaktari, kwa sababu masilahi ya anayehamishiwa si bora zaidi kisharia kuliko masilahi ya anaeyechukuliwa kiungo hicho, madhara hayaondoshwi kwa madhara, hakuna kujidhuru wala kudhuru katika Uislamu, na kunatosha katika hili masilahi sahihi. Madhara madogo ya kawaida na kiada na kisharia hayazuii kujuzu huku katika kuruhusiwa kama yatajulikana awali na kukawezekana kuyavumilia au kuyazuia kivitendo au kimaana kwa anayehamishwa kiungo chake, na wanaoeleza haya wawewataalamu wa kimatibabu na waadilifu.

Kutoka kithibitisho cha kimaandishi kutoka katika jopo la madaktari kabla ya kuhamisha kiungo kwa kujua vidhibiti hivi na kuwapa wahusika wa pande mbili- anayehamisha na anyehamishiwa- kabla ya kufanya upasuaji, pamoja na kuwa jopo hili limebobea na lisiwe chini ya madaktari watatu waadilifu na pasiwe na yeyote kati yao ana masilahi na operesheni hii.

Sharti kiungo kinachohamishwa kisiwe kinapelekea kuchanganya koo kwa hali yeyote.

Dalili ya hayo kama ifuatavyo:

Ama dalili ya kusema kujuzu kuchukua kiungo kutoka kwa mtu mwingine katika njia tuliyoielezea ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu” [Al-Baqara:173]na neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.” [Al-Maida:3]. “naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni,” [Al-Anaam:119]. Na muongozo wa dalili katika Aya hizi tukufu, kwamba zote zimekubaliana juu ya kuondoa uharamu katika hali ya dharura inayoelezewa katika Aya hiyo, na mgonjwa akihitaji kuhamishiwa kiungo basi anakuwa katika hukumu ya mwenye dharura; kwa sababu uhai wake upo hatarini kama kwa mgonjwa aliyefeli figo, na kuharibika kwa moyo na mifano yao katika viungo muhimu katika mwili wa mwanadamu.

Na ikiwa hali ni kama hivyo, basi kunaingia katika kuenea kuvua kulikotajwa, basi kunaruhusiwa kuhamishiwa kiungo ([13]).

Ama dalili ya kujuzu mwanadamu kutoa kiungo chake kwa anayehitaji ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi” [Amaida:32], aya hii inajumuisha kuongoa kuangamia, na ndani yake kunaingia kujitolea kiungo kwa ndugu yake ili amuokoe na kuangamia([14]) kwa sababu anathibitisha kuwa amehuyisha nafsi ya ndugu yake.

Vilevile Mwenyezi Mungu Mtukufu amemsifu mwenye kumtanguliza ndugu yake kabla yeye mwenyewe kwa chakula au kinywaji au mali; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.”[Al-Hash’ri:9}, ikiwa hilo katika mambo madogo, Mwenye kumtanguliza ndugu yake kwa kiungo chake au sehemu yake ili amuokoe na kuangamia kulikothibitishwa, hapana shaka kwamba hilo ni bora kusifiwa, vilevile kitendo hiki kinazingatiwa kuwa limeruhusiwa kisharia na lenye kupongezwa([15]). 

Kanuni kuu za Sharia hazipingi hilo; yale tuliyoyathibitisha kujuzu yanakubaliana na kanuni ya Madhara huondoshwa, na kanuni ya Dharura huruhusu yaliyokatazwa, na kanuni jambo likiwa limebana hupanuliwa([16]); Mgonjwa amedhurika kwa kuharibikiwa na kiungo au kukikosa, pia sehemu yake huzingatiwa kuwa sehemu ya dharura, na ana dhiki na mashaka; inaweza ikifikia hali yake daraja ya kuhofia kuangamia kama hali ya kufeli kwa figo([17]).

Sharia imejuzisha kujitibu kwa kuvaa Hariri kwa mwenye kuwa na muwasho, na imeruhusu kujitibu kwa kutumia dhahabu kwa muhitaji, kunachukuliwa kipimo cha kujitibu kwa kuhamisha viungo vya mwanadamu kwa hilo kwa kuwepo haja inayopeleka hilo katika yote ([18]).

Na hivi ndivyo hufanya mizani ya usawa kati ya uharibifu; huondolewa madhara makubwa kwa madhara madogo, na huchaguliwa nafuu zaidi ya shari mbili ([19]), vikikutana viwili viharibifu huepukwa madhara makubwa kwa kufanya madhara madogo ([20]). Katika masuala yetu haya kumekutana kati ya uharibifu wa kuchukua kiungo hai na kutokea maumivu, na kati ya uharibifu wa kuangamia kwa aliyehai aneyepewa kiungo, na hapana shaka kwamba uharibifu wa kuangamia aliyehai anayepewa kiungo ni mkubwa kulingo uharibifu unaopatikana kwa mtu anayejitolea, hapa hutanguliwa, kwa sababu huu ni uharibifu wenye madhara makubwa na hatari zaidi ([21]).

Rai nyingine:

Baadhi ya wanazuoni wameharamisha kuhamisha viungo visivyo kimoja kimoja kwa kujitolea, na upambanuzi wa hilo utakuja katika sehemu ifuatayo; kwa sababu walioharamisha kuhamisha viungo vya mwanadamu kwa mwanadamu mwingine, wameharamisha katika hali zote, hakuna tofauti kati ya kuhamisha kutoka kwa mtu aliyehai au maiti; katika viungo kimoja kimoja au vinginevyo, kwa kuuza au kujitolea, kwa hivyo tumechelewesha kauli yao na kutaja dalili zao baada ya kumaliza kutaja kauli za wanaojuzisha kuhamisha viungo kutoka kwa mtu aliyehai kwa kujitolea au kutoka kwa maiti kwa sharti zake na dalili zao; ili kufupisha na kutorudiarudia.

Sehemu ya Tano

Kuhamisha viungo vya mwanadamu aliyefariki na kuvipandikiza kwa mtu aliyehai

Miongoni mwa aina za kuhamisha viungo ni kuwa anayehamishwa ni mwanadamu aliyefariki na anayehamishiwa mwanadamu aliye hai, hakujuzu kuhamisha kiungo cha maiti kwa kukiuza; kwa sababu kuuza ni tawi la kumiliki, na mwili wa maiti si milki ya mtu yeyote ili kujuzu kuuza.

Ama kutoa kiungo cha maiti kwa idhini, hilo linashurutizwa kuwepo hali ya dharura au haja za kisharia kwa namna kunajuzu kuhama kutoka asili ya kuzuiwa kwenda kujuzu kwa kuvua; kwa kuondoa madhara na kuepuka uharibifu, heshima ya viungo vya maiti hakuzuii mtu aliyehai kunufaika navyo; kwa kutanguliza muhimu zaidi juu ya muhimu, na dharura hulalisha marufuku, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” [Al-Anaam:145].

Na idhini inatoka kwa maiti kabla ya kifo chake kwa kuusuia, au kutoka kwa ndugu zake au mawalii wake baada ya kifo chake, na kuzingatia wasia wa marehemu au ruhusa ya mawalii wake ni suala la nidhamu tu, mzunguko wa kujuzu kufaidika na viungo vya maiti ni kuwepo hali ya dharura ya kisharia inayohalalisha kilichokatazwa, lakini ili jambo lisiachwe bila yavidhibiti na madaktari wasifikishwe mahakamani, tumesema ulazima wa kuwepo wasia kabla ya kifo au idhini ya mawlii baada ya kifo katika njia za sera za kisharia kwa kufikia masilahi na kuondoa ufisadi.

Na limekuja hili katika tanzu za Fiqhi za zamani ambalo linapeleka kusema kujuzu, yakiwemo maneno yao katika mlango wa jeneza kuhusu kupasua tumbo la mwanamke aliyefariki akiwa na mimba na mtoto wake yupo hai anatikisika tumboni kwake, na atakapokufa mtoto tumboni mwa mama yake na mama yungali hai, na kupasua tumbo la maiti ili kutoa mali aliyoimeza kabla ya kufa kwake.

Katika hili wanasema wanazuoni wa Fiqhi wa Hanafi: “” Mwanamke mjamzito amefariki na mtoto wake yupo hai anatikisika, atapasuliwa tumbo lake ubavu wa kushoto, na atatolewa mtoto wake, na kwa kinyume- kama mtoto atakufa tumboni mwa mama yake na mama akawa yuhai-, lau maiti akiwa amemeza mali ya mtu mwingine- si mali yake- na akafa- na hakuacha katika mali yake kinachoweza kulipa mali hiyo- je, anapasuliwa? Hapa kuna kauli mbili: ya kwanza ndio; kwa sababu pamoja na kwamba ni kuheshimu mwanadamu kuko juu kuliko kulinda mali lakini ameondosha heshima yake kwa kufanya kosa”([22]).

Na katika Fiqhi ya Malik: kwamba hupasuliwa tumbo la maiti ili  kutoa mali ambayo ameimeza akiwa hai, sawasawa mali yake au mali ya mtu mwingine, wala hapasuliwi ili kutolewa mtoto japo kuwa anategemewa kuishi.

Katika Mukhtasar Khalil  na sherehe yake ya Shekhe Alyesh: “Na hupasuliwa tumbo la maiti kwa sababu ya mali aliyoimeza akiwa hai na akafa hali yakuwa mali hiyo imo tumboni mwake, sawasawa mali ni yake au ni mwingine.

Wala halipasuliwi tumbo la maiti kwa sababu ya mtoto mchanga aliyetumboni mwake anaetegemewa kuishi, kwa sababu usalama wake una mashaka, basi haivunjwi heshima yake, na mali imehakikiwa kutoka kwake([23]).

Na katika Fiqhi ya Shafi: Atakapofariki mwanamke na tumboni mwake kuna mtoto aliye hai, hupasuliwa tumbo lake, kwa sababu hilo ni kumbakiza mtu hai kwa kuharibu sehemu ya maiti, kukafanana na mwenye kudharurika kula nyama maiti, na hili kukitegemewa maisha ya mtoto wa tumboni baada ya kumtoa, ama kama hakutegemewa kuishi, hapasuliwi tumbo lake lakini hatozikwa mpaka mtoto afariki.

Katika sherehe ya Albajiirimiy: “Na kumeharamishwa kufukua kaburi kabla ya kuoza isipokuwa kwa dharura kama kuzikwa bila ya kuoshwa, au akizikwa mwanamke mwenye mimba na kitoto kinachotarajiwa kuishi  kwa kuwa na miezi sita na zaidi, basi hupasuliwa tumbo lake na kutolewa, na kupasuliwa kwake ni lazima kabla ya kumzika,kama hakitarajiwi kuishi basi hapasuliwi, lakini hatozikwa mpaka kife kitoto kisha atazikwa, na yaliyosemwa kwamba awekewe kitu tumboni kwake ili afe ni makosa makubwa, tahadharini”([24]).

Na kuhusu maiti kumeza mali wamesema: Maiti akimeza vito vya mtu mwingine, na mwenye vito vyake akavitaka, litapasuliwa tumbo lake na kuchukuliwa vito, isipokuwa kama atadhamini mmoja wa warithi, na kama vito ni vya kwake basi hapasuliwi; kwa sababu amevitumia wakati wa uhai wake, havifungamani na haki ya mirathi.

Katika sherehe ya Jamal kusherehesha Almanhaj: “Na kama atameza mali yake mwenyewe na akafa, hafukuliwi kwa kuitumia kipindi cha uhai wake, au mali ya mtu mwingine na mwenyewe akaidai, atafukuliwa na kupasuliwa tumbo lake na itatolewa na kurudishwa kwa mmiliki wake, lau warithi wake watamdhamini kama ilivyoelezewa katika majmou kwamba warithi wakimdhamini hapasuliwi tumbo lake, na anaunga mkono maneno yao kuwa atapasuliwa tumbo maiti ikiwa hakuna dhamana ana alichokiacha, kwa maana anapasuliwa tumbo pamoja na kuacha mali, vilevile anapasuliwa pamoja na dhamana ya warithi, kama ilivyo katika eda, muda wa udhamini wa mmoja wa warithi au mtu mwingine  kunakuwa haramu kumfukua na kupasua tumbo lake; kwa kusimama mtu sehemu yake, ili kulinda kuvunja heshima ya maiti, na yanajibiwa yaliyo katika Al-majmou kwamba hakuna kuuunga mkono, kwa sababu dhamana imethibiti katika mali aliyoacha badala kwamba ipo hatarini kuharibiwa kinyume na iliyo katika dhima inayotokana na dhamana([25]).

Fiqhi ya Hambali inasema: Maiti akimeza mali akiwa hai, ikiwa  ni milki yake hapasuliwi tumbo lake;  kwa sababu ameitumia katika uhai wake ikiwa kidogo, ikiwa na thamani kubwa atapasuliwa tumbo lake na kutolewa mali hiyo ili kuhifadhiwa isipotee na ili iwanufaishe warithi ambao wanafungamana nayo haki yao kwa ugonjwa wake, na ikiwa mali ya mtu mwingine na akaimeza kwa ruhusu ya mmiliki wake basi hiyo inakuwa katika hukumu ya mali yake kwa sababu mmiliki wake ametoa ruhusa ya kuitumia, na akimeza kwa kulazimishwa, kuna kauli mbili, ya kwanza: Hapasuliwi tumbo lake na itachukuliwa katika mali yake, ya pili: Atapasuliwa ikiwa nyingi; kwa sababu katika hilo kuna kuondoa madhara kwa mmiliki wa mali kwa kurudisha mali yake, na kwa maiti kuondosha dhima yake, na kwa warithi kulinda mali walioachiwa.

Na katika Al-Iqnaa sherehe ya Albahouty: “(Na ikianguka mali katika kaburi kwa kiasi kinachojulikana, au aliitupa mmiliki wake litafukiliwa kaburi”) na itachukuliwa mali hiyo kwa yale yaliyokuja  “kwamba Mughira bin Shuubah aliweka pete yake katika kaburi la Mtume S.A.W.  kisha akasema: pete yangu akaingia na akaichukua, alikuwa anasema: Mimi ndiye niliyekaribu zaidi na zama za Mtume, na akasema Ahmad: Mchimba kaburi akisahau jembe lake kaburini kunajuzu kufukuliwa kaburi. Mwisho; kwa kufungamana na haki ya Mola wake na kitu chake pamoja na kutodhuru katika kuichukua.

 (au akimeza mali ya mtu mwingine bila ya idhi yake na ikabaki katika mali yake kama pete, na akaitaka mmiliki wake, hafukuliwi na italipwa katika mali aliyoicha) kwa kulinda heshima yake pamoja na kutoleta madhara.(kukiwa na uzito kulipa mali aliyomeza maiti kwa kutoacha mali na mfano wake, litafukuliwa kaburi na atapasuliwa tumbo lake na kutolewa mali na kupewa mmiliki wake, ikiwa haijalipwa thamani yake, kwa kutotoa warithi wake au mtu mwingine thamani ya sanda au mali  kwa mmiliki wake, na kama itatolewa basi hafukuliwi kwa yaliyotangulia. Na kama atameza mali ya mtu mwingine kwa idhini ya mwenye mali itachukuliwa maiti itakapooza ) kwa sababu mmiliki wake ndiye aliyemmilikisha mali yake kwa idhini yake, wala hafukuliwi maiti kabla ya kuoza kwa yaliyotangulia, wala haidhaminiwi na kwa mali yake aliyoicha  wala mmiliki wake hatoidai kwa warithi wake, kwa sababu yeye ndie aliyemmilikisha. Na akimeza mali yake mwenyewe hafukuliwi kabla ya kuoza;kwa sababu hilo ni kutumia mali yake mwenyewe katika uhai wake kunafanana na kuiharibu, isipokuwa kama atakuwa anadaiwa, atafukuliwa na kupasuliwa tumbo lake na kutolewa mali na litalipwa deni lake, kwa sababu katika hilo kuna kumuokoa na dhima  ya deni”([26]). 

Na muhtasari wa yaliyotangulia: kwamba Madhehebu mawili ya Hanafi na Shafii yanajuzisha kupasua tumbo la maiti sawasawa kwa kutoa mtoto wa tumboni aliyehai au kutoa mali, na kwamba Madhehebu mawili ya Malik na Hanbal wanaruhurusu kupasua tumbo la maiti kwa mali lakini si mtoto wa tumboni.

Ikiwa wanazuoni wa Fiqhi- Allah awarehemu- wameeleza kujuzu kupasua tumbo la maiti kwa kutoa vito vya thamani vya mtu mwingine alivyovimeza maiti, basi kujuzu kuhamisha viungo vya maiti ni bora ili kuokoa nafsi inayoheshimiwa ambayo ina heshima kubwa kuliko mali([27]).

Na miongoni mwa kauli za kifiqhi zilizotolewa ushahidi: kwamba baadhi ya Madhehebu ya watu wa elimu- Allah awerehemu- miongoni mwa wanazuoni wa Fiqhi wamesema kunajuzu kula nyama ya mwanadamu maiti kwa dharura.

Amesema Imamu An-Nawawy katika Majmou: “Na kunajuzu kwa mtu aliyedharurika kumuua kafiri mwenye kuupiga vita Uislamu na mwenye kuritadi na kuwala na halina tofauti hilo, ama mzinifu aliyeoa na mpiganaji na mwenye kuacha Swala kwao kuna kauli mbili: Iliyo sahihi zaidi na ameipitisha Imamu wa Haramayn na mtunzi na Jamhuri: kuna juzu, Amesema Al-Imamu: Hakika si vingine tumekataza kuuwa watu hawa kwa kutegemeza kwa mtawala ili asilifanye bila ya kufanya shura, na udhuru huu hauwajibishi kuharamisha wakati wakuthibitisha dharuara ya aliyedharurika. Ama aliyedharurika akimpata mtu ambaye kunapasa kisasi kwake basi kunajuzu kwake kumuua kwa kisasi na kumla sawasawa ameletwa na mtawala au hapana, kwa kile tulichokitaja katika masuala yaliyotangulia, Albaghwiy ameliezea hili na wengineo, ama aliyedharurika ikiwahakupata isipokuwa mwanadamu maiti aliyehifadhiwa, basi kuna kauli mbili iliyo sahihi zaidi na inayojulikana zaidi: kunajuzu, na njia hii ameipitisha mtunzi na wanazuoni waliowengi, na ya pili ina kauli mbili amezielezea Al-Baghwy sahihi ni kujuzu; kwa sababu heshima ya aliyehai inasisitizwa zaidi, na ya pili hakujuzu; kwa kupasa kumlinda na si kwa kitu chochote([28]).

Na inajulikana kwamba mgonjwa ambaye amefikia hali ya dharura kama kufeli kwa figo, na moyo ambavyo vinamuweka mtu kwenye tishio la kifo, wanazuoni hawa wa Fiqhi wameeleza kujuzu kula ya maiti asiehifadhiwa na mwenye kuhifadhiwa pamoja na kwamba kula kunawajibisha kukata viungo, basi kujuzu kuhamisha viungo na kujitolea kunakowajibisha kubaki kwa mtu kuwa hai ni bora zadi, na heshima ya mtu aliye hai ni bora kuliko ya mtu aliyefariki katika asili na katika suala letu hili pia([29]).

Shekhe Jad Al-Haqq anasema katika Fatwa yake inayofungamana na suala hili: “Na kutoa hukumu ya hilo na kuijengea: kunajuzu kupasua tumbo la mwanadamu aliyeifariki na kuchukua kiungo cha mwili wake au sehemu ya kiungo ili kukihamisha katika mwili mwingine wa mwanadamu aliyehali, ambaye madaktari wana asilimia kubwa ya kufaidika mwanadamu huyu na kiungo alichohamishiwa, kwa kuchunga masilahi sahihi waliyoyana wanazuoni wa Fiqhi wasemao kujuzu kupasua tumbo la mwanamke aliyefariki akiwa na mimba na mtoto akawa anatikisika na kukawa kunatarajiwa kuishi baada ya kukitoa, na kwa kufanyia kazi kanuni ya dharura zinahalalisha yaliyokatazwa, na madhara makubwa yanaondoshwa na madhara madogo, ambayo ameitegemeza katika Qur`ani na Hadithi za Mtume S.A.W. kwani miongoni mwa matumizi yake kama ilivyotangulia ni kujuzu kula nyama ya maiti ya mwanadamu wakati wa dharura ili kulinda uhai wa aliyehai asife njaa, kulikotangulizwa juu ya kulinda heshima ya maiti kwa kufanyia kazi kanuni mbili za kuchagua shari yenye ahueni zaini kati ya shari mbili, na vikikutana viwili nyenye kuharibu kitaepukwa kikubwa chao kwa madhara kwa kufanya chenye madhara madogo. Na ikiwa kunajuzu kula nyama ya maiti ya mwanadamu kwa dharura, basi kunajuzu kuchukua baadhi ya viungo vyake na kuvihamishia kwa mwanadamu mwingine aliyehai kwa kulinda uhai wake muda wakuhakikiwa kuwa na faida kwa asilimia kubwa, na haja yake ya kiungo anachohamishiwa ([30]). 

Na kwa ufupi: Kwamba ruhusa ya kuhamisha viungo vya mwanadamu kutoka kwa mtu aliyefariki kwenda kwa mtu aliyehai hapana budi kuchunga vidhibiti vifuatavyo:

Kuwa anayechukuliwa kiungo amehakikiwa kuwa amekufa kifo cha kisharia; kwa kutoka uhai kamili, kwa kusimama kufanya kazi kabisa viungo vyote vya mwili, na kuwa muhali kurudi katika uhai mara nyingine kwa ushahidi wa wataalamu waadilifu ambao humjua mtu aliyepoteza maisha, kiasi kwamba anaruhusiwa kuzikwa, nakuwa ushahidi huu wa kimaandishi na wenye saini zao.

Kuwepo hali ya dharura au haja za kisharia, kiasi kwamba hali ya ugonjwa anayehamishiwa kiungo ni mbaya kwa kuendelea,  na hakuna cha kumuokoa kwa mtazamo wa madktari na kumpatia masilahi ya dharura ambayo hayana njia isipokuwa kuhamisha kiungo kutoka kwa mwanadamu mwingine.

Kuwa marehemu anaechukuliwa kiungo chake ameusia hilo katika uhai wake, akiwa na nguvu zake kamili kiakili bila ya kulazimishwa kifedha au kimaana, na anajuwa kwamba yeye anausia kiungo maalumu kutoka katika mwili wake kwenda kwa mwanadamu mwingine baada ya kifo chake, au idhini ya mawalii wake kwa hilo.

Kutokuwa kiungo kilichohamishwa kutoka kwa maiti kwenda kwa mtu aliyehai kinapelekea kuchanganya koo kwa hali yeyote, kama viungo vya uzazi na vinginevyo, na hii ni kama ilivyo katika kuhamisha kiungo kutoka kwa ailyehai kwenda kwa aliye hai.

Kuwa uhamishaji katika kituo cha afya bobezi kilichopitishwa na serikali na kilichoidhinishwa kufanya hivyo moja kwa moja bila ya kupeana pesa kati ya pande mbili, na hili linakuwa sawasawa kwa tajiri na masikini, kwa kiasi vinawekwa vidhibiti, Kwa namna kunawekwa vidhibiti vya usawa kati yao katika kupewa huduma za matibabu, wala hatungulizwi mmoja wao isipokuwa kwa muktadha wa dharura  za kimatibabu tu ambazo zinapelekea kuokoa kutoka katika madhara yaliothibitishwa au kifo na kuangamia kwa mgonjwa. 

Rai Nyingine

Na kuna kundi kubwa la Wanazuoni wasasa([31]) linakataza kuhamisha viungo kwa hali yeyote sawasawa kutoka kwa aliyehai au aliyekufa, kwa njia ya kuuza au kutoa bure, rai yao wameitolea dalili kutoka katika Qur`ani na Hadithi, dalili za kiakili na kanuni za kifiqhi, na wakazitilia mkazo kwa kauli za wanazuoni wa Fiqhi wa zamani.

Dalili ya Kwanza:

Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.” [Al-Baqara:195] pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu: ““ Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni” [Annisaai:29]”. Wanaokataza wamesema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametukataza katika Aya hizi mbili kujiua na kujiingiza wenyewe katika maangamizi, na amakataza mwanadamu kujiua mwenyewe au kumuua mtu mwingine. Na mtu kwenda kujitolea sehemu ya mwili wake, hilo kiuhalisia ni kufanya harakati za kujiangamiza katika njia ya kutafuta uhai wa mtu mwingine, na hilo halitakiwa kwake, na neno kuangamia katika Aya ni tamko linalokusanya  kila linalopelekea kuangamia, na kukata kiungo chake mwenyewe kunawajibisha kuondoa manufaa yake ni moja ya mambo ambayo yanapelekea kuangamia, na mazingatio ni kwa kuenea tamko sio sababu iliyohusishwa kwa kile walichokitaja wanazuoni wa elimu ya Usuulul Fiqhi, na kukataza katika Aya ya pili kunakusanya sababu zote ambazo zinapelekea katika kilichokatazwa, nako ni kuua nafsi, na miongoni mwa sababu hizi zilizokatazwa ni mtu kuingia makubalino na mtu mwingime ili ajitolee sehemu katika mwili wake kwa mwenzake([32]).

Na hili linajadiliwa kwa njia zifuatazo:

Njia ya kwanza:  Hatufuati njia yao katika mawili haya; kwa sababu sisi tumeweka sharti katika kujuzu kuhamisha kiungo, maisha ya mwenye kujitolea kiungo hicho kutokuwa katika hatari ya kuangamia, na kusema kuwa kujitolea kiungo wakati wa uhai kunapelekea kuangamia  hakukubaliwi isipokuwa kwa ushahidi wa madaktari wazoefu,  na wao hawasemi hilo kabisa, hapo yametoka katika sehemu ya mjadala.

Njia ya pili: Tumekubali kusihi kwa dalili zao, lakini tunasema kwamba dalili hizo ni maalumu kuliko madai, kwa sababu zinahusiana na wakati wa uhai, ama baada ya kifo hazihusiki.

Njia ya tatu: Kugeuza njia za kutolea dalili kwao, na hilo ni: kwamba mtu akikataa kiungo alichojitolea mtu mwingine ambacho kinategemewa kuokoka kwake- kwa idhini ya Mwenyezi Mungu- anazingatiwa kuwa anajiingiza katika maangamizi, ni haramu kwake kukataa kwa njia hii, na kukubali kwake kunakuwa ni kisharia na wajibu kwake([33]).

Dalili ya pili:

Wametoa dalili pia kwamba Shetani amesema kama ilivyosimulia Qur’an tukufu: “basi watabadili aliyoumba Mwenyezi Mungu.”[Annisaai:119], Aya hii inakusanya kuhamisha viungo, kwa sababu inaingia katika kuenea kubadilisha alivyoumba Mwenyezi Mungu, kama kuhamisha jicho au figo au moyo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, inakusanya pia kuwakata uume watumwa kama walivyokuwa wakifanya makhalifa kwa watumwa wao ili waingie vyumba vya wanawake wao. Haya yote ni kubadili alichoumba Mwenyezi Mungu inayajumuisha Aya tukufu.

Na kukata masikio ya wanyama hawayajumuishi na hilo, kwa sababu mazingatio ni kuenea kwa tamko si kuhusu sababu, na hii ni kanuni ya kiusul inayojulikana([34]).

Dalili hii imejadiliwa kwa kuzuia kuchukua maana ya dhahiri ya Aya; kwa sababu vitu vingi vilivyothibitishwa kujuzu ni ibara ya kubadilisha alivyoumba Mwenyezi Mungu, kama kutahiri, kukata kucha na nywele, kubadilisha mapitio ya maji na kuondosha milima na kutengeneza barabara na mengineyo katika mambo mengi tunayokubaliana kujuzu kwake lakini kidhahiri ni kubadili alivyoumba Mwenyezi Mungu([35]).

Hivyo tunasema kwamba viungo vipo nje ya Aya hii; kwa sababu hili linakuwa kwa kupatikana dharura au haja ya hilo.

Dalili ya tatu:

Wametolea dalili pia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba” [Al-Israa:70], Na njia ya dalili ya Aya hii: Ni kwamba Aya hii tukufu imetoa dalili juu ya Mwenyezi Mungu kumkirimu mwanadamu, na kumkirimu huku kunakusanya kipindi cha uhai wake na umauti wake, na kutoa kiungo katika mwili wa mwanadamu kunaenda kinyume na kumtukuza huku mwanadamu sawasawa katika uhai wake au baada ya kifo([36]).

Hili linajadiliwa kwamba madaktari wanalinda maisha ya mtu anaejitolea kiungo akiwa hai kwa kiasi kikubwa, na katika operesheni hii ya kuhamisha kiungo hakuna hata kitu kidogo kinachoenda kinyume na kumtukuza Mwanadamu kulikotajwa katika aya hii.

Bali katika kuhamisha huku kuna kumtukuza mwanadamu kihisia na kimaana, ama kumtukuza kihisia; kwa sababu kiungo hiki badala yakuzikwa mchangani na kuoza kitaendelea kubaki katika mwili wa mwanadamu kinamsaidia katia kumtii Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake. Ama kumtukuza kimaana; Ndani yake kuna malipo mema kwa kujitolea kwa kuwa ameondoa tatizo la ndugu yake Muislamu, hii ikiwa kuhamisha kutoka kwa Muislamu, ama kuhamisha kutoka kwa kafiri hii si aina ya makusudio ya kumtukuza kwake, bali kumdhalilisha ndiko kulikokusudiwa kisharia, Nakuchezea mwili wake ni haramu ikiwa hakuna sababu yeyote, ama kukiwa na sababu basi hakuna ubaya kama ilivyo hapa, pamoja kutokubali kwamba operesheni ya kuhamisha viungo ni kuuchezea mwili; kuuchezea mwili kunakuwa baada ya mateso na hilo haliwi katika kuhamisha viungo.

Dalili ya nne:

Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Jabir Allah amuwieradhi, kwamba Mtume alipohamia Madina, alihamia pia Al-Tufayly bin Amr Al-Dousy pamoja na mtu wa kabila lake, wakaichukia madina, akaumwa akawa na hofu kubwa, akachukua mshale wenye mapana ya ncha akajikata pachipachi za vidole, mikono yake ikatiririka damu nyingi mpaka akafariki, Al-Tufayl bin Umar akamuona ndotoni akiwa na umbo zuri akiwa amefunika mikono yake, akamuuliza: nini amekufanyia Mola wako? Akasema: Amenisamehe kwa kuhamia kwa Mtume S.A.W. akamuuliza: Mbona nakuona umefunika mikono yako? Akasema: Nimeambiwa: Hatukutengenezei ulichokiharibu. Al-Tufayl akamsimulia Mtume S.A.W. akasema Mtume S.A.W.: “Ewe Mola na kwa mikono yake msamehe”([37]), Hadithi hii imetujuza kwamba mwenye kuchukua hatua katika kiungo chake kwa kujitolea au kwa jambo lingine, basi atafufuliwa siku ya kiama akiwa hana kiungo hicho kama malipo yake; kwa sababu kauli yake: “Hatukutengenezei ulichokiharibu” haifungamani na kuua nafsi bali inafungamana na jeraha kwa kujikata kwake, pia mwenye kujitolea jicho atafufuliwa akiwa jicho moja, na mwenye kujitole moyo au pafu hatorudishiwa kiungo hicho([38]).

Dalili hii inajadiliwa kutoitumia kwa yaliyotajwa;  kwamba hakuna uthibitisho kuwa mwenye kujitolea kiungo chake atafufuliwa akiwa na upungufu, bali ina simulizi ya ndoto iliyohadithiwa kwa Mtume S.A.W. akamuombea mtu wake alihadithiwa kisa hicho, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi.

Dalili ya tano:

Wametolea dalili pia Hadithi ya Asmaa bint Aboubakar Allah amuwie radhi amesema: Alifika mwanamke kwa Mtume S.A.W. akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nina mtoto wa kike mwanamwali amepatwa na surua nywele zake zimeanguka, je, niziunge? Akasema: “Amemlaani Mwenyezi Mungu mwenye kuungwa nywele na muungaji wake”([39]), kutolea dalili Hadithi hii: Ni kwamba Hadithi imetoa dalili ya uharamu wa mwanamke kunufaika na nywele za mtu mwingine nazo ni sehemu za huyo mtu nwingine, ndio inazingatiwa asili ya kukataza kunufaika na sehemu za mwanadamu, japo kuwa manufaa hayo hayamdhuru mwenye kuchukuliwa sehemu hiyo([40]).

Al-Sayyid Abdillah bin Al-Sideek Al-Ghamary anasema: “ Mwanamke mmoja alilalamika kwa Mtume S.A.W. kwa maradhi yaliyompata binti yake, na akamtaka amruhusu kufanya hilo, akafahamisha vitu viwili:

Kwamba kujitibu kwa kuhamisha kiungo, hakujuzu bali na mfanyaji wa hilo amelaaniwa.

Kwamba mwenye kupatwa na ugonjwa ukaathiri nywele zake au kiungo chake hakujuzu kwake kukiunga kutoka kwa mtu mwingine.

Na sababu ya hilo: kwamba kunabadilisha Umbo aliloumba Mwenyezi Mungu,na kuhadaa, na ndani yake kuna ukataji kiungo nako kumeharamishwa, na mwanadamu kuchukua hatua katika kitu asichomiliki, na ni kinyume na heshima ya mwanadamu”([41]).

Na hili linajadiliwa kwa njia mbili:

Njia ya kwanza: kwamba kuunga nywele kunazingatiwa kuwa ni masilahi ya ziada, tofauti na viungo ambavyo vinazingatiwa kuwa ni masilahi ya lazima, kunaharamishwa la kwanza na kunahalalishwa la pili kutokana na mahitaji yake.

Njia ya pili:

Kwamba kuunga nywele kulikotajwa katika Hadithi kunapelekea uharibifu na kumdhuru mtu mwingine, nako ni mwanamke kumdanganya mume wake, kama ilivyo katika Hadithi, kinyume na kuhamisha viungo ambako kunakusanya kuondoa uharibifu.

Ama kauli ya Shekhe Al-Maghary kwamba kutibu kwa kuhamisha viungo kunapelekea laana kwa mtendaji wake, haikubaliki kwa mambo mawili:

La kwanza: Kwamba lilothibiti katika elimu ya Usuul kwamba kipimo cha usawa hupitishwa katika hukumu, kama kipimo cha usawa (Al-Qiyas) cha mvinyo kwa pombe katika uharamu, ama laana na ghadhabu na mfano wa hayo hayafanyiwi kipimo cha usawa (Al-Qiyas); na kwa sababu muweka sharia pekee ndiye ajuaye anaestahiki hilo, Muweka sharia amemlaani mwenye mwanamke mwenye kunyoa nywele za uso na hakumlaani mzinifu, pamoja na kwamba zinaa ni mbaya kuliko kunyoa nywele za uso ama kipimo cha kuhamisha viungo kwa kunyoa nywele za uso na kuunga nywele na tatuu havikubaliki.

Ya pili: Imethibiti katika elimu ya Usuul Al-fiqhi kwamba kuunganisha hukumu katika tawi kunaruhusiwa kwa sababu ya asili ya tawi, na sharia ilipomlaani mwanamke mwenye kunyoa nywele za uso na mwenye kuchora tatuu  kuwaita kuwa wanabadilisha alichoumba Mwenyezi Mungu, imejulisha kwamba sababu ya hilo ni kunyoa nywele za uso au kuchora tatuu, hivyo hakufai kusema kwamba kuhamisha kiungo ni kama kunyoa nywele za uso au kuchora tatuu, na mtendaji wake amelaaniwa.

Dalili ya Sita

Ni Hadithi za kukataza kukata viungo, miongoni mwa Hadithi hizo ni Hadithi ya Burayda Allah amuwie radhi, amesema: “Mtume S.A.W. alikuwa akimpa mtu uongozi wa jeshi au kundi dogo la jeshi, anamuusia yeye hasa kumcha Mungu na kuwausia alionao katika Waislamu mambo ya kheri, kisha akasema: Piganeni kwa jina Mwenyezi Mungu katika njia ya Mwenyezi Mungu, wauweni waliomkufuru Mwenyezi Mungu, piganeni vita wala msipetuke mipaka wala msifanye khiana wala msikate viungo wala msiue vitoto vichanga...”([42]), kisha akasema: Piganeni kwa jina Mwenyezi Mungu katika njia ya Mwenyezi Mungu, wauweni waliomkufuru Mwenyezi Mungu, piganeni vita wala msipetuke mipaka wala msifanye khiana wala.. “ Muongozo  wa dalili: kwamba Hadithi imetoa dalili ya kuharamisha kukata viungo, na kukata viungo si haramu kwa wanyama tu, na kwa kubadilisha umbile la mwanadamu kwa njia ya mchezo na kulipa kisasi, bali kunakusanya kukata sehemu yeyote au kiungo cha mwanadamu au mnyama au kumjeruhi akiwa hai au akiwa amekufa bila ya ugonjwa([43]).

Hili limejibiwa kwamba kukata viungo kunakuwa wakati wa uvamizi; ikiwa mwanadamu kwa hiari yake na akamtaka daktari kutoa kiungo chake kumpa ndugu yake au rafiki yake, hapa kutoa kiungo hakuitwi kukata kiungo([44]).

Na ikialazimishwa kwamba katika kuhamisha kiungo kuna ukataji wa viungo, basi jibu ni: Uharibifu wa kukata kiungo unapingana na uharibifu wa kuangamia mgonjwa anayehitaji kiungo, kunapasa kuzingatia uharibifu mkubwa nayo ni kuangamia kwa mgonjwa, kisha panaangaliwa uharibifu mdogo kwa kufuata kanuni ya kisharia: Yakikutana mawili yenye kuharibu huepukwa kubwa kwa kufanya dogo lake.

Vilevile ukiondoka ubaya wa kukata viungo katika elimu ya atonomia kwa masilahi yaliyopo , basi kuondoka ubaya katika kuhamishaviungo ni bora na sahihi zaidi.

Dalili ya Saba

Pia wametolea dalili Hadithi iliyopokelewa kuhusu Uislamu kuheshimu maiti, kutoka kwa mama wa Waumini Aisha R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Kuvunja mifupa ya maiti ni kama kumvunja akiwa hai”, Hadithi hii imepokelewa na Ad-Darqatniy katika “Ithmu”([45]),

Na njia ya dalili: Hadithi imeeleza kuwa mtu aliye hai ni haramu kuvunja mifupa yake au kukata viungo vyake, vilevile maiti kwa sababu yoyote, isipokuwa aliye hai kwa sababu ya idhini ya Mtungaji Sharia([46]).

Katika Hadithi Sahihi kutoka kwa Abu Hurayra kwamba Mtume S.A.W. anasema: “Kukaa mmoja wenu katika kaa la moto likaunguza nguo yake na kumaliza ngozi yake ni bora kwake kuliko kukaa juu ya kaburi”([47]), Al-Sayyid Abdallah Al-Ghamary anasema: “Huu ni ndio ukomo wa kuheshimu maiti, na kuacha kuikera au kushusha heshima yake, vipi wathubutu baadhi ya watoa Fatwa kuruhusu kutoa kiungo katika mwili wake bila ya dalili?!”([48]).

Hili linajibiwa kwamba kwa dhahiri maana yake: Maiti ana heshima yake kama heshima ya aliye hai, mwili wake haushambuliwi kwa kukata mifupa au kitu kingine katika ambayo yaondoa heshima bila ya dharura au masilahi yaliyothibitishwa.

Na maana hii ni ya dhahiri ndiyo iliyotajwa na Wanazuoni wa Hadithi katika kubainisha sababu ya hadithi hii, kwamba wachimbaji kaburi walitaka kuvunja mifupa ya maiti pasi na masilahi yeyote.

Na kwa maana hii inaendana na makusudio ya Uislamu kuhusu kuchunga masilahi yaliyothibitishwa, na kupata madhara madogo ili kuepusha madhara makubwa ([49]).

Pia linajadiliwa katika njia mbili kama ifuatvyo:

Njia ya kwanza inasema kunajuzu kwa hali yeyote: Kwamba kufananisha kuvunja mfupa wa maiti na mfupa wa aliye hai ni katika asili ya uharamu, si katika kipimo chake, kwa dalili ya kutofautiana dhamana na kisasi, katika kuishambulia maiti kuna madhambi na kuadhiriwa, hakuna kisasi na fidia, na kutofautiana katika yanayopasa kumlinda aliye hai kwa yasiopasa kumlinda maiti.

Njia ya pili inayosema kujuzu kuhamisha viungo kutoka kwa kafiri tu:  Hadithi hii inafungamana na muumini kama ilivyokuja wazi katika riwaya nyingine, na kafiri damu yake hailindwi si akiwa hai au maiti “Isipokuwa akiwa Dhimiy au Mustaaman” kunajuzu kutumia viungo vyake hata kama atadhurika na hilo.

Dalili ya Saba

Wametolea dalili pia Hadithi ya Ibnu Abbas R.A. yeye na baba yeke, amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Usidhuru wala usijidhuru”([50]), njia ya dalili: kwamba kukata kiungo kwa mtu anayejitolea kwa mwingine, kuna madhara kwa upande wa sharia na mwili kwa mtu anayekatwa, ama kiupande wa Sharia ni kauli ya Mtume S.A.W.: “Hakika damu zenu, mali zenu, ni haramu kwenu”,  ama kwa upande wa mwili, hapana shaka kwamba ndani yake kuna kupunguza umbo la asili, na kuna madhara, na madhara yoyote yanaingia katika katazo na ni haramu kufanya hivyo([51]).

Hili linajibiwa kuwa uharamu unaondoka katika hali hii; kwa sababu dalili ya uharamu ni madhara na kupunguza kiungo cha mwanadamu, na hii ipo katika hali kama kukata kiungo hicho bila ya jambo la msingi, ama kukiwa na jambo la msingi kama tulilo nalo basi si haramu, na hili lipo katika picha ya kuokoka kukazama kwa kutupa mazao ya mtu mwingine, katika hali hii kuharibu mazao hayo si haramu, kwa sababu tunatanguliza kuokoa maisha ya watu juu ya kuharibu mazao, vilevile katika jambo letu hili, kukiwa na mtu anamatatizo ya figo, mtu mwingine akataka kujitolea figo lake moja ili aokoe maisha yake, katika hali hii uharamu huondoka[52], japokuwa hatukubali kwamba operesheni ya kuhamisha kiungo ni uharibifu wa moja kwa moja kwa mtu anayehamishwa; hii kwa sababu madaktari hawafanyi hili kutoka kwa mtu ambaye atakufa kwa kuhamisha kiungo chake, katika hali hii haturuhusu hilo, hivyo basi Hadithi inatoka katika utata huu.

Dalili ya Nane

Wametolea dalili pia Hadithi ya Jabir bi Abdillah R.A. yeye na baba yake kwamba Mtume S.A.W. alimwambia mtu mmoja: “Anza kwa kujitolea sadaka mwenyewe, kikibaki kitu basi wape familia yako, kikibaki kitu basi wape ndugu zako, kikibaki kitu basi fanya hivi na hivi  …”([53]), na njia ya dalili; kwamba Mtume S.A.W. ameweka misingi ya utaratibu katika kugawa, akamuelekeza kuanza na yeye mwenyewe, kisha mke wake na watoto wake, kisha ndugu, hakupasi kujidhuru mtu kwa masilahi ya mtu mwingine.

Ikiwa hili katika matumizi, basi inakuwa bora zaidi mtu kutojidhuru kwa maisha ya mtu mwingine, hata kwa dharura kubwa kiasi gani, na sisi tumeamrishwa kufuata mtini za kisharia([54]).

Hili linajadiliwa kwamba Mwenyezi Mungu Amemsifu anayempendelea ndugu yake kwa chakula au kinywaji au mali, ikiwa haya katika mambo madogo madogo, basi vipi mwenye kumtanguliza ndugu yake kwa kiungo au sehemu ya kiungo ili aokoe maisha yake, hapana shaka hilo ni bora zaidi kusifiwa, vilevile kufanya hivi japo si wajibu kama wasemavyo wanaokataza, isipokuwa kunajuzu kisharia, bali ni katika mambo ya kujitoa yanayopendeza.

Ama kutoa dalili kwa Hadithi hii kwamba mtu ameamrishwa kutojidhuru kwa maisha ya mtu mwingine kwa dharura yeyote, tunajibu kwamba, sisi haturuhusu kama mtu anayejitolea atakuwa amejiweka kwenye matatizo kama atajitolea kiungo kama ilivyotangulia.

Bali inawezekana kujibiwa hilo kwa kugeuza dalili hiyo: kwa kusema kwamba mwanadamu akitaka kujitolea kiungo ajitolee mwenyewe, kama kukiwa na madhara basi asijitolee, ama kukiwa hakuna madhara basi Hadithi haimgusi kabisa.

Dalili ya Tisa

Wametoa dalili kwamba viungo vya mwanadamu si milki yake, ni milki ya Mwenyezi Mungu, ameviumba kwa ajili yake ili anufaike navyo, hivyo hanauwezo wa kuvitoa kwa kuuza au kujitolea, na sharti ya mtu kutumia kitu ni kuwa milki yake au amemilikishwa na mmiliki wake mwenyewe.

Hivyo Mwenyezi Mungu ameharamisha kujiua na ameahidi kukaa motoni milele kwa anayejiua; kwa sababu amekusudia kutumia kitu ambacho si milki yake, ni milki ya Mwenyezi Mungu hivyo akawa amedhulumu kwa hilo.

Hili linajibiwa kuwa maneno haya si sawa, na hayana dalili inayokubalika, kwa sababu kitu ambacho si milki ya mwanadamu ni uhai wake na roho yake, hivyo hakujuzu kujiua wala kujiingiza katika maangamizi isipokuwa kwa dharura kubwa, kama jihadi na kujitetea ambavyo Uislamu umeamrisha, ama mwanadamu kwa upande wa viungo vyake yeye ndiye mmiliki wake, na anaweza kufanya jambo ambalo halimsababishii madhara makubwa.

Hivyo mwanadamu ameruhusiwa kufanya jambo lenye kheri za dunia na akhera katika mwili wake, na ruhusa ya kuhamisha viungo ina kheri  kwa akhera kutokana na thawabu ambazo anazipata kwa kuondosha shida kwa Muislamu na kumfanyia wema.

Pamoja na kuchunga kwamba Dharura huhalalisha yaliyokatazwa kama tulivyosema hapo awali, kwa kunufaika na mwili wa maiti pia([55]).

  Dalili ya Kumi

Wamesema: kwamba kuondoa uharibifu ndio makusudio ya Sharia, katika kujitolea kiungo kuna uharibifu mkubwa ambao unazidi masilahi yake, kwa sababu ndani yake kuna uharibifu wa manufaa ya viungo vya mwili unaohamishwa, jambo ambalo linaweza kupelekea maangamizi, au kunawezekana kupelekea kuzembea kutekeleza ibada na wajibu na kuacha baadhi ya amri kwa hiari yake([56]).

Hili linajibiwa kwamba kuhamisha viungo ili kujuzu kunashartizwa kutosababisha maangamizi kwa mtu anayehamishwa, na kutopelekea madhara makubwa, na hili linakubaliwa kwa ushahidi wa madaktari waaminifu,  daktari mtaalamu wa hilo akipitisha  kwamba kuhamisha kiungo kutoka kwa mwanadamu kwenda kwa mwingine kwa lengo la matibabu, na hili halina madhara kabisa kwa anayechukuliwa kiungo chake; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, na kitamnufaisha anayehamishiwa, basi linajuzu kisharia([57]), hivyo basi, dalili hii inakuwa imetoka katika maudhui ya mjadala.

Dalili ya Kumi na Moja

Wamesema kuwa heshima ya mali ni ndogo kuliko heshima ya roho, na Mtume S.A.W. ameamrisha kuchunga heshima za watu, hivyo ni vizuri zaidi kuchunga viungo vyao([58]).

Hili linajibiwa, kwamba heshima ya mali inakubaliwa kwa idhini ya mmili wake, vilele kuhamisha viungo.

Dalili ya Kumi na Mbili

Wamesema: Hakujuzu kukata viungo vya mwanadamu kama kulivyo hakujuzu kukata kipande cha nyama kwa kuwa vyote hivyo ni katika viungo vya mwili([59]).

Hili linajibiwa kwamba kukata nyama kumejengewa katika uharamu wa kushirikiana; kwa kuwa linapelekea uharibifu wa zina, na sababu hii haiwi katika kuhamisha viungo, kisha kufanya kipimo cha Sharia katika hilo si sahihi.

Dalili ya Kumi na Tatu

Wamesema kwamba kuhamisha viungo kunagongana na kanuni ya kisharia ambayo inasema kwamba, madhara hayaondoshwi kwa madhara, na madhara hayaondoshwi kwa mfano wake. Katika suala letu ni kwamba madhara yanaondoshwa kwa mtu anayehamishiwa kiungo kwa madhara mengine yanampata anayejitolea kiungo([60]).

Hili linajibiwa kwamba kanuni hii haijibiwi kwa kusema kuna juzu; kwa sababu katika sharti zake, ni kutosababisha maangamizi kwa mtu anyehamishwa kiungo au madhara.

Dalili ya Kumi na Nne

Wametolea dalili pia kwa kanuni: Kwamba kinachojuzu kukiuza kunajuzu kukitoa bure, na kisichojuzu kukiuza hakijuzu kutolewa bure([61]); wanajuzisha kuhamisha viungo wanakubali kwamba viungo havijuzu kuviuza, na kanuni imejulisha lkiwa kisichojuzu kukiuza hakijuzu kukitoa bure, hivyo basi, hakujuzu kujitolea viungo vya mwanadamu si kwa aliye hai kama yeye na hata baada ya kifo([62]).

Hili linajibiwa kwamba kanuni hizi ni kwa asilimia kubwa, Wanazuoni wa Madhehebu ya Shafi wamezitoa kanuni hizi katika baadhi ya mambo: Kama mjakazi aliyewekwa rehani,akitakiwa kuzaa na aliyemuwekea rehani hali ya kuwa yeye masikini, au akamuacha huru kunajuzu kwake kumuuza kwa sababu ya dharura, na hakujuzu kumtoa bure si kwa aliyeweka rehani wala kwa mwingine([63]), katika sura hii kunajuzu kumuuza kwa dharura na hakujuzu kumtoa bure; hii ni kwa sababu kuuza kunaondosha uzito, kinyume na kutoa bure, pamoja na kwamba yote mawili ni kumilikisha, isipokuwa katika kuuza kuna kumiliki na ziada na hiyo ndiyo badala ambayo inaondosha uzito.

Na katika suala la kuhamisha viungo ambalo lipo mbele yetu, hili ndani yake kuna dharura au haja inayopelekea sehemu ya dharura, na ambalo inafikia kuondosha madhara au mahitaji ni kutoa bure si kuuza, hivyo kunabainika kuwa kila kanuni ina vinavyovuliwa, na katika hili kunavuliwa suala la kuokoa roho na kuondosha uzito na mateso.

Kauli za Wanazuoni wa Fiqhi ambazo wamezitolea ushahidi

Wanaoharamisha kuhamisha viungo wametolea ushahidi kauli zinazoendana na \Madhehebu yao katika kauli za Wanazuoni wa Fiqhi([64]) zikihukumu uharamu wa kunufaika na viungo vya maiti kwa heshima yake, na hakuna haki ya kukata kutuoa kiungo kumpa mwingine akiwa katika madhara, pia hakusihi kukata kiungo chake mwenyewe na kula, na haifai kwa mtu mwingine kukata kiungo cha mwenzake na kula; kwa sababu hili haliruhusiwi kwa ruhusa wala haizingatiwi ridhaa yake na wala halitekelezwi.

Maiti hakujuzu kufanyiwa hilo; kwa sababu anapata maumivu kama mtu aliye hai, kumuharibu na kuvunja heshima yake hakujuzu.

Ibnu Abdeen katika wanazuno wa Fiqhi ya Madhehebu ya Abou Hanifa amesema: “Mtu akiambiwa na mwingine kata mkono wangu na ule, si halali; kwa sababu nyama ya mwanadamu si halali kwa kuondoa heshima yake”([65]).

Na katika Sharhi Al-Mukhtasara Al-Khalil - cha Mawaq katika vitabu vya Madhehebu ya Imamu Malik: “Dharura inaweza kuondoshwa kwa kutokula nyama ya mwanadamu” Albajy amesema: Hakujuzu kwa mtu aliyedharurika kula nyama ya mwanadamu aliyefariki japo akihofia kifo”([66]).

Na katika Minhaj wa Sharhihi cha Khatib Al-Shirbiny katika vitabu vya Madhehebu ya Shafi: “Ni haramu moja kwa moja kwa mtu kujikata sehemu ya mwili wake na kumpa mtu mwingine mwenye dharura; kwa sababu kumpa mtu sehemu ya mwili wake si kukata baadhi nakubakisha kikubwa.

Ufafanuzi: hii kama huyo mwingine si Mtume, na ikiwa ni mtume si haramu bali ni wajibu, na ni haramu kwa mtu aliyedharurika kujikatia kiungo kutoka kwa mnyama kwa yaliyotangulia”([67]).

Na katika Al-Iqnaa wa Sharhihi cha Al-Bahtawiy katika vitabu vya madhehebu ya Hanbaly: “Na ni haramu kwa wanyama yaliyoharamu kwa wanadamu” kwa kuingia kauli ya Mwenyezi Mungu: (Mmeharimishiwa nyamafu)[Al-Maidah, 3] na kwa maana ya Hadithi: “Tumehalalishiwa maiti mbili na damu mbili([68])”mwisho([69]).

Ndani yake pia: Aliyedharurika asipopata kitu chochote halali au haramu, haiwi halali kwake kula sehemu ya mwili wake, kwa sababu anakiharibu ili apate kisicho na uhakika” ndani yake pia: “Aliyedharurika asipopata kitu isipokuwa nyama ya mwanadamu anayemwagika damu, si halali kwake kumuua au kukata kiungo chake, awe Muislamu, kafiri dhimiy au anayeishi kwa kupewa amani; kwa sababu anayelindwa akiwa hai ni kama aliyedharurika, hukujuzu kwake kumkata mtu mwingine ili aishi yeye” mwisho([70]).

Tunapozingatia kauli za Wanazuoni zilizotangulia, tunakuta kwamba zimekusanya yafuatayo:

Sababu ya kuharamisha kunufaika na viungo vya mwanadamu ni kuwa kunawajibisha kuvunja heshima yake.

Hili linajibiwa kwa yaliyotangulia tulipojibu dalili yao katika kauli ya Mwenyezi Mungu: (Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini...).

Kutojuzu kukata kitu chochote katika mwili wa mwanadamu ili kula, pia hakujuzu kujikata mwenye na kula nyama yake. Hili linajibiwa kwa njia mbili:

Njia ya kwanza: Hili halijumuishi baada ya kufa - kumkata mtu mwingine - kwa kutokuwepo uharibifu unaopatikana kwa kumkata akiwa hai.

Njia ya pili: kwamba dalili hii inapingana na maelezo ya kujuzu kukata baadhi ili kubakisha yote, kama iliyvyo katika kukata mkono ulioharibika na uvimbe na mfano wake katika vitu vinavyoharibu mwili. Kauli yao ya kujuzu kukata katika njia hii ni dalili ya kuzingatia kwao hukumu ya kujuzu kukata ili kuokoa nafsi, na hili ndilo linalopasa katika kuhamisha viungo.

Sababu ya kutojuzu kunufaika au kukata au kufanya chochote kinachofanana na hayo kwa kuwa maiti anapata maumivu kama aliye hai, kwa yale yaliyo katika kuharamisha kuvunja mifupa ya maiti.

Hili linajibiwa kwa yaliyotangulia katika kujibu Hadithi iliyokuja katika kuvunja mifupa.

Kwa mujibu wa haya: Kuhamisha viungo kutoka kwa mtu aliye hai au maiti kwa kujitolea, si kibiashara, kunajuzu kisharia, zitakapopatikana sharti maalum ambazo zinaweka mbali jambo hili na kumchezea mwanadamu ambaye Mwenyezi Mungu amkemtukuza, na kutomfanya kipuli cha biashara, bali lengo linakuwa kusaidiana katika wema na ucha Mungu na kupunguza maumivu kwa mwanadamu, na kama hakutapatikana njia nyingine ya matibabu itakayozuia kuangamia kwa mwanadamu, na madaktari wataalamu, waaminifu wakapitisha kuwa njia hii inaleta manufaa ya uhakika na haitoleta madhara kwa mtu aliyechukuliwa kiungo chake na haitoathiri afya yake, maisha yake na kazi zake kwa sasa au baada ya muda, na kama tulivyoelezea yote hapo awali katika vidhibiti vya kisharia katika suala la kuhamisha viungo. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.

Sura ya sita

Hukumu ya kuhamisha na kupandikiza viungo vya uzazi

Mfumo wa uzazi wa mwanamume unajumuisha Uume, korodani, tezi ya kibofu, na vilengelenge shahawa, na maarufu ni kuhamisha korodani.

Kazi ya korodani ni kutoa homoni zinazohitajika kuunda viungo vingine vya mfumo wa uzazi wa mwanamume.

Pia hutoa homoni ya kiume kutoka hatua za mwanzo za ujauzito, na hii ili kutengeneza viungo vingine vya mfumo wa uzazi wa mwanamume, pia huunda mbegu za kiume pale mwanamume anapobalehe kutoka kwenye seli za msingi zilizopo kwenye korodani, ambazo hubeba sifa za kiurithi ambazo seli hizo za msingi zimerithi kutoka kwenye korodani, korodani inafanya kazi ya kiwanda kinachozalisha mbegu za kiume kupitia ushawishi wa Homoni kwa mada za msingi (seli ya mwanzo inayozalisha mbegu zilizokomaa) iliyoko kwenye korodani.

Korodani hii ikihamishiwa kwa mtu mwingine basi tunahamisha kiwanda chenye mashine, vifaa na malighafi zake kwenda sehemu nyingine, na jukumu la aliyehamishiwa litakuwa ni kuendesha kiwanda tu, yaani hatakuwa na jukumu katika kuhamisha jenitik zilizobebwa na watoto wake, bali badala yake atasaidia katika kuhamisha kromosomu za Kinasaba ambazo amezirithisha mtu aliyehamishwa korodani kwenda kwenye kizazi cha mtu aliyehamishiwa korodani.

Ni kana kwamba tumerutubisha yai la mke wa mtu ambaye amehamishiwa korodani kwa mbegu ya mwanamume mwingine aliyehamishwa korodani lake, ikipandikizwa korodani kati ya wanaume, basi hapo tunasaidia kuchanganya koo.

Kuhusu mfumo wa uzazi wa mwanamke, umegawanyika kati ya sehemu ya ndani na nje, sehemu ya ndani ina ovari mbili (viyai vya uzazi), moja upande wa kulia na nyingine upande wa kushoto wa mrija wa uzazi, uterasi na uke, ovari huunganishwa na uterasi kwa mshipa mnene wa upande wa kulia na kushoto, nayo ni mifuko ambayo ina idadi maalumu ya mayai wakati wa kuzaa, ambayo ni,  idadi ya mayai ndani ya ovari ambayo yanakuwa yameundwa kabla ya mwanamke kuzaliwa kutoka tumboni mwa mama yake.

Lau tukihamisha ovari kutoka kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwanamke mwingine, basi kwa kufanya hivi tunakuwa tumehamisha vyote, yakiwemo mayai yaliyomo ambayo yanabeba sifa za kinasaba ambazo mwanamke ambaye ovari imetolewa amerithi kutoka kwa wazazi wake kwenda kwa mwanamke mwingine aliyehamishiwa ovari, na katika hili kuna shaka ya kuchanganya koo.

Ama viungo vingine vya uzazi, kama vile uume, uterasi, mirija na uke, ni kama viungo vingine vya mwili, kama vile moyo, figo na ini, kwa kuwa haviathiri koo([71]).

Kulingana na yaliyotangulia, kinachoonekana ni kwamba hakujuzu kuhamisha viungo vya uzazi vinavyosababisha kuchanganya koo.

Sura ya Saba

Hukumu ya kuhamisha kiungo kutoka kwa mnyama kwenda kwa mwandamu

Suala hili lipo kwa kunufaika kwa mnyama kwa meno yake, mifupa yake au viungo vyake vingine, kama moyo, ini, figo na vinginevyo, na kunufaika kwa jino, mfupa na mfano wao kunawezekana na kupo kiuhalisia, ama kuhamisha viungo hai, kama moyo na ini, hivi japokuwa mpaka sasa havijafanikishwa isipokuwa vinafanyiwa tafiti na huwenda vikawafanikishwa hapo baadaye.

Katika hili kunatakikana kutofautisha kati ya sura mbili:

Kwanza: Kunufaika na viungo vya mnyama aliyetwahara, naye ni aneyeliwa kihalali, hakuharamishwi kujitibu kwa viungo vyake; kwa kuwa dalili imejumisha uhalali wa kujitubu kwa wanyama hao.

Kujitibu kwa viungo vya mnyama katika mtindo huu ni halali kama kujitibu kwa vitu vilivyohalali; kwa kuwa vyote ni twahara, na kwamba kila kinachojuzu kunufaika na sehemu zake pamoja na kukitumia kama chakula kwa kukata mifupa, basi kujuzu kunufaika nacho kwa viungo vyake na kubaki kwake ni bora zaidi([72]).

Swali hili waliliibua Wanazuoni wa Fiqhi wa zamani, wakataja aina zake: Kwamba mfupa wa mwanadamu ukivunjika, basi kunatakikana kuungwa kwa mfupa uliotwahara, na hakujuzu kuunga kwa mfupa ulio najisi isipokuwa wakati wa dharura, kama vile ikiwa haukupatikana isipokuwa mfupa huo, pia kunajuzu kuweka jino la mnyama twahara sehemu iliyotoka jino la mwanadamu.

Imekuja katika Badaaii Al-Saanii cha Kassany katika vitabu vya Madhehebu ya Hanafi: “Kama litang’oka jino lake ni makruhu kuchukua jino la maiti na kuliweka sehemu yake kwa makubaliano ya Wanazuoni, vilele ni makruhu kurudisha jino lililongóka kwa Madhehebu ya Hanafi na Muhammad Allah awarehemu, lakini litachukuliwa jino la mnyama halali na kuwekwa sehemu yake, na Abou Yussuf Allah Amrehemu amesema: hakuna ubaya kuweka jino lake na makruhu kuweka jino la mwingine”([73]).

Na katika Hashiya Al-Dusouqy Alaa Sharhi Al-kabeer katika vitabu vya Madhehebu ya Malik: “Litakapo ng’oka jino kunajuzu kulirudisha na kuliunga na kamba ya dhahabu au fedha, na kumejuzu kulirudisha; kwa sababu maiti ya mwanadamu ni twahara” vilevile kunajuzu kuweka badala yake jino la mnyama halali, ama mnyama aliyefariki kuna kauli mbili: Kujuzu na kutojuzu, kwa kufuata kauli ya pili basi ni wajibu kulitoa wakati wa kila suala kama hakutokuwa na uzito, kama kutakuwa na uzito basi hapana”([74]).

Na katika Al-Majmouu An-Nawawy: “Mfupa wake ukivunjika kunatakikana kuunga kwa mfupa uliotwahara, watu wetu wamesema: Hakujuzu kuunga kwa mfupa najisi pamoja na kuweza kupatikana uliotwahara utakaokaa sehemu yake, akiuunga na mfupa ulio najisi, kutaangaliwa- akiwa anahitaji kuuga na hakupata uliotwahara basi anapewa udhuru, na ikiwa hakuuhitajia na akapata ulio twahara atapata dhambi, na kunapasa kuutoa kama hatohofia kuharibika kiungo, akihofia kuangamia au kuharibika au kuondoka manufaa ya kiungo hakupasi kuutoa kwa usahihi wa njia mbili”([75]).

Ibnu Qudama Al-Hanbaly amesema: “Akiuunga mfupa wake kwa mfupa ukaungika, kisha akafa, basi hautolewi mfupa huo ukiwa ni twahara, na ukiwa najisi na kukawezekana kutolewa basi utatolewa, kwa sababu huo ni najisi inayowezekana kuondolewa bila ya madhara”([76]).

Pili: kunufaika na viungo vya wanyama najisi, naye ni mfu anayeliwa nyama yake, na asiyeliwa, asili katika aina hii ni Uharamu; kwa kuwa kuweka najisi katika mwili kunawajibisha kubatilika Swala na ibada nyinginezo ambazo zin\ sharti la twahara, lakini tunaangalia katika hali ya dharura… je, kunajuzu kuhamisha ua hakujuzu?

Mwenye kuzingatia maelezo ya Wanazuoni wa Fiqhi anakuta kwamba yanajulisha kwamba asili, ni haranu kunufaika na kujitibu kwa najisi, bali kunatakikana kutegemea vilivyotwahara katika hili, akikosa, atarudi kujitibu kwa vilivyonajisi, katika hili ni lazima kupatikana sharti mbili:

Ya kwanza: Dharua au haja ambayo itamuweka katika hilo, na itakadiriwa kwa kiasi chake, kwa kujitibu kwa najisi hii, hili litathibitishwa na ushahidi wa madaktari wataalamu.

Ya pili: Kutopatikana kiungo kitakachokaa sehemu yake katika viungo twahara, au vinginezyo([77]).

Hivyo basi, kusema kuwa kunajuzu kujitibu na kunufaika na aina hii ni kinyume na asili, na hapanabudi kuhakikishwa sharti mbili zilizotangulia.

Ibnu Abdeen Al-hanafy amenukuu katika Hashiyat Radd Al-Muhtaar Alaa Al-Daar Al-Mukhtaar kutoka katika hazina za Fatwa katika mambo yenye kuharibu Swala: Mfupa wake umevunjika, ukaungwa kwa mfupa wa mbwa na hautolewi isipokuwa kwa maumivu, Swala inajuzu([78]).

Na katika Iqnaa wa Sharhihi cha Al-Bahouty katika vitabu vya Madhehbu ya Hanbali: “Akishona jereha lake, au akaunga mguu wake na mfano wake, kama mkono kwa uzi au mfupa najisi ukaungika na akapona hakumlazimu kuuondosha, akihofia madhara, kama ugonjwa na mengineyo pia akihofia kuharibika kiungo au kuangamia yeye mwenyewe; kwa sababu ya kulinda roho na viungo na madhara ni wajibu”([79]).

Pia angalia nukuu ya Imamu An-Nawawy iliyotajwa hapo juu.

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi.

Sehemu ya Pili

Masuala yanayofungamana na Utafiti huu

Sura ya kwanza: Masuala katika hukumu ya kuhamisha damu.

Sura ya pili: Hukumu katika kuhamisha seli za shina.

Sura ya tatu: Musuala yanayofungamana na kufa kwa ubongo.

Sura ya nne: Hukumu ya kurudisha viungo vilivyokatwa kwa hadi au kisasi.

Sura ya kwanza

Masuala katika hukumu ya kuhamisha damu.

Wanazuoni wote wamekubaliana kuwa damu inayotiririka ni najisi, na ni haramu kunufaika nayo; na hii ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: (Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu)[Baqarah, 173], Qurtuby amesema: “Wanazuoni wamekubaliana kuwa damu ni haramu na najsi, hailiwi wala haitumiwi katika kitu chochote”([80]). Imamu An-Nawiwy amesema katika Majmou: “Na dalili ya unajisi wa damu inayoonekana, na sijui kama kuna tofauti ya hili kwa Muislamu yeyote, isipokuwa alichosema Muandishi wa Al-Hawy kutoka kwa baadhi ya wasemaji kuwa yeye amesema: Ni twahara, lakini wasemeji hawahesabiwi katika makubaliano na kutofautiana, kwa Madhehebu sahihi ambayo Wanazuoni wa Usuul wanayafuata katika watu wetu na wengineo, hasa katika masuala ya Fiqhi”([81]).

Lakini wakati mwingine utoaji damu unahitajika ili kuwatibu wagonjwa waliopoteza damu, iwe kwenye ajali au upasuaji, ikiwa hawatofanyiwa hilo basi uhai wao utakuwa hatarini, na hapa kunakuwa kujitolea damu na kuihamisha kunajuzu na hakuna ubaya, na dalili ya hili ni:

Kwanza: Kwamba hali ya dharura imetolewa katika uharamu ulioelezewa katika Aya, kama kauli yake Mwenyezi Mungu: (Naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipo kuwa vile mnavyo lazimishwa)[Al-An’aam, 119]. Mgonjwa akihitaji kuhamishiwa damu basi hilo litakuwa katika hukumu ya dharura; kwa sababu maisha yake yapo hatairini, damu hata kama ni najisi, na hakujuzu kuitumia, isipokuwa kunajuzu kuitumia wakati wa dharura.

Pili: katika kauli ya Mwenyezi Mungu: (Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote)[Al-Maidah, 32] neno kuokoa linajumuisha uokoji wowote, na hapana shaka kwamba mweye kujitolea damu kwa ndugu yake; hakika amefanya hivyo ili kumuokoa na umauti.

Tatu: Katika kuruhusu kuhamisha damu kuna kuwafanyia wepesi waja na kuwahurumia wagonjwa, na kuwapunguzia maumivu, na haya yote ni misismamo ya malengo ya Sharia, tofauti na kuharamisha kuhamisha damu, kwani ndani yake kuna uzito na jambo ambalo linapingana na dalili ya matini za kisharia; na anasema Mwenyezi Mungu: (Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu)[Al-Maidah, 6].

Nne: kwamba Kuhamisha damu katika hali ambazo tumezizungumzia na mfano wake kunazingatiwa kuwa zinaingia katika amri ya kujitibu ambayo imekuja katika Hadithi ya Mtume S.A.W.: “Jitibuni enyi waja wa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu hakuweka ugonjwa isipokuwa ameuwekea dawa, ipokuwa uzee”([82]).

Tano: Kwamba miongoni mwa kanuni za Sharia za Kiislamu, ni kwamba dharura huhalalisha yaliokatazwa, Madhara huondoshwa, Uzito huleta wepesi. Na zote hizi zinahukumu kujuzu kuhamisha damu kwa kujitolea, kwa sababu ya dharura na haja.

Sita: Ni yale waliyoeleza baadhi ya Wanazuoni wa Fiqhi waliotangulia na wa sasa katika kujuzu kujitibu kwa damu; miongoni mwa hayo ni yaliyokuja kutoka kwa Abduraaziq katika kitabu chake kutoka kwa Ibnu Jurayj amesema: “Nimemsikia Ataa anaulizwa na mtu aliyeambiwa anywe damu ili apone maumivu ya ini, akamruhusu kufanya hivyo. Akasema Ibnu Jurayj: Mwenyezi Mungu Ameharamisha, akasema: Dharura, Ibnu Jurayj akamwambia: Hilo ikiwa anajua kuwa linaponya, lakini hajui, na akamtajia maziwa ya punda akamruhusu  kunywa kwa kujitibu”([83]).

Mwanazuoni Ibu Abdeen amenukuu katika Radd Al-Muhtaar An Baadh kutub Hanafiya kwamba kunajuzu kwa mgonjwa kunywa mkojo, damu, na mfu kwa ajili ya dawa, atakapoambiwa na daktari Muislamu kwamba hilo linaponya, na hakupata kilicho halali kitakachoponya([84]).

Kutokana na yote yaliyotangulia, kuhamisha damu na kujitolea kumpa mtu mwingine kunazingatiwa kuwa ni katika mbambo yanayopendeza kisharia; kwa kuwa ndani yake kuna kuokoa roho, na hili ni pamoja na kuchunga sharti zifuatazo:

Mgonjwa kuwa anahitaji hilo kwa ushahidi wa madaktari waadilifu.

Kuwa na ugumu wa mbadala wa tiba hiyo.

Kutosababisha madhara kwa anayejitolea.

Kutosheka na kiasi ambacho kinaweza kuondosha dharura ambayo inakadiriwa kwa kiasi chake([85]).

Ama kuuza damu, Wanazuoni hawakutofautiana juu uharamu wake, Imamu Ibnu Al-Mundhir amesema katika kitabu chake cha Al-Ijmaa katika mlango wa biashara: Kwamba Wanazuoni wamekubaliana juu ya kuharamisha alichoharamisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa mfu, damu na nguruwe([86]); hivyo basi, hakujuzu kuuza damu kutokana na yafuatayo:

Kwanza: Mwenyezi Mungu Ameharamisha damu, na akasisitiza hili kwa kuongeza kuharamisha aina zake, hilo likajulisha kuharamisha kunakusanya njia zote za kunufaika na damu, na kuuza na kunufaika nayo ni haramu.

Pili:Hadithi iliyokuja katika sahihi Al-Bukhary katika kukataza thamani ya damu kwa Matini maalumu, imepokewa kutoka kwa Aun bin Abi Juhayfa amesema: Nimemuona baba yangu akimnunua mtumwa mpiga chuku, akamuamrisha kuvunja chombo chake, nikamuuliza, akasema: Mtume S.A.W. amekataza thamani ya mbwa, thamani ya damu na amekataza kuchorwaa na kuchora tatuu, na kula riba na mwenye kutoa riba na amemlaani mwenye mwenye kuchonga masanamu([87]).

Hafidh Ibnu Hajara amesema katika Fathi: “Wametofautiana kilichokusudiwa katika thamani ya damu, wakasema baadhi yao: Malipo ya kupiga chuku, na wengine wakasema: Ni kama ilivyo kwa dhahiri yake, na kilichokusudiwa ni kuharamisha kuuza damu kama kulivyoharamishwa kuuza mfu na nguruwe, na hilo ni haramu kwa makubaliano ya Wanazuoni, nakusudia kuuza damu na kuchukua thamani yake”([88]).

Tatu: Hadithi iliyopokelewa katika Sunan Abi Dawoud kutoka kwa Inbu Abbas R.A. yeye na baba yake amesema: Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amekaa katika nguzo, akasema: akanyanyua macho yake mbinguni, akacheka, kisha akasema: “Mwenyezi Mungu amewalaani mayahudi” mara tatu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaharamishia mafuta ya wanyama waliochinjwa, wakayauza na wakala thamani yake, na hakika Mwenyezi Mungu akiwaharamishia watu kula kitu, huwaharamishia kula thamani yake”([89]).

Katika Hadithi hii kuna mambo mawili:

La kwanza: kwamba Mtume S.A.W. amewakemea mayahudi kuuza alichokiharamisha Mwenyezi Mungu, ikasihi kwamba sharia itakapoharamisha kitu, huharamisha kukiuza na kula thamani yake, isipokuwa itakapokuja matini kuhusisha kitu katika hilo basi husimamia hapo.

La Pili: Mtume S.A.W. amesisitiza hili kwa kuliweka wazi katika nusu ya pili ya Hadithi kwa kusema: “...hakika Mwenyezi Mungu akiwaharamishia watu kula kitu, huwaharamishia kula thamani yake”, Imamu An-Nawawy ameelaza kusihi kwa Hadithi hii katika zaidi ya sehemu moja katika kitabu chake cha Al-Majmou([90]).

Ikatoa dalili katika kuharamisha huku tahamani ya damu.

Nne:Asili ya kitu kinachouzwa kuwa ni twahara, kunajuzu kunufaika nacho, na damu ni najisi; hivyo basi imekatazwa thamani yake.

Aliyedharurika kuhamishiwa damu asipopata mtu wa kujitolea, na akampata mtu atakaempa damu kwa malipo, kunajuzu kwake kumlipa, na kunajuzu kutoa pesa ili kupata damu; kwa sababu amedharurika amehalalishiwa kilichoharamishwa ambacho ni damu, hivyo kunaruhusiwa kwake njia ya kuipata nayo ni kununua ambako ni bora, na anayechukua pesa yeye peke yake ndie anayepata dhambi.

Amesema mtunzi wa Mughny Al-Muhtaj: “Kama kulivyoharamu kuchuku malipo katika kilichoharamishwa, ni haramu kukitoa isipokuwa kwa dharura, kama kumkomboa aliyetekwa, kumpa mshairi ili asimshambulie kwa mashairi, na dhalimu ili kuepuka dhuluma yake, na hakimu ili ahukumu kwa haki, hakuwi haramu kutoa katika haya”([91]).

Vilevile kunajuzu kwa mwenye kutoa damu kuchukua pesa si kwa njia ya mbadala bali kwa njia ya kuondosha umiliki, na Mwezi Mungu ni mjuzi zaidi.

Sura ya pili

Suala la kuhamisha Seli za shina

Seli za shina ni seli zisizo na upendeleo na zisizo maalumu na zina uwezo wa kugawanyika na kuongezeka ili kutoa aina tofauti za seli maalumu na kuunda tishu tofauti za mwili, Seli hizi hubakia katika umbo hili hadi zipokee viashirio maalumu vinavyozisukuma kukua na kuwa seli zenye upendeleo.

Wanasayansi hivi karibuni wameweza kutambua, kutenganisha, na kukuza seli hizi; Kwa lengo la kuzitumia kutibu baadhi ya magonjwa. Seli hizi zinaweza kupatikana  kwa njia ya kijusi wakati kikiwa katika hatua ya mpira wa vijidudu, au kuharibika kwa mimba katika hatua yeyote ya ujauzito, au kupitia kondo la nyuma au kitovu, au kupitia  watoto au watu wazima, au kwa njia ya kuunganishwa kwa kuchukua seli kutoka kwa seli ya ndani.

Kupata, kukua na kutumia seli hizi; Kwa madhumuni ya matibabu, au kufanya utafiti wa kisayansi kunaruhusiwa ikiwa hakuleti madhara kwa mtu aliyechukuliwa kutoka kwake, inajuzu kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu, ikiwa zimepatikana kutoka kwa mtu mzima kwa idhini yake, pia kuzichukua kutoka kwenye kondo au kitovu, au kutoka  katika ya kijusi cha mimba iliyotoka wenyewe au kwa sababu ya kisharia ikiwa wazazi watatoa ruhusa, na pia katika hali ya chanjo za ziada kutoka kwenye  miradi ya watoto wa chupa ikiwa zitapatikana na wakajitolea wazazi wawili.

Hakujuzu kupata seli za shina kupitia njia ya haramu, kama vile kutoa mimba kwa kukusudia bila sababu ya kisharia, au kwa kurutubisha yai la mwanamke kwa makusudi na mbegu ya mtu kando, au kwa kuzichukua kutoka kwa mtoto, hata kama kwa idhini ya mzazi/mlezi wake; Kwa sababu mzazi/mlezi hana haki ya maamuzi katika yanayowahusu wale walio chini ya ulezi wake isipokuwa katika yale yenye manufaa ya wazi kwake.

Masuala yanayofungamana na kufa kwa ubongo

Ukweli wa kifo kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu: Roho kutengana na mwili, na kutoka roho kunajulikana kwa ishara za mwili za kifo.

Wanazuoni wa Fiqhi walitaja katika vitabu vyao baadhi ya dalili ambazo kifo kinajulikana kwazo, Imamu Ibn Qudamah amesema katika Al-Mughni: “Ikiwa hali ya maiti inashukiwa, zingatia kuonekana kwa dalili za kifo, kama vile kulegea kwake miguu, mgawanyiko wa viganja vyake, kuinamisha pua yake, kupanuka kwa ngozi ya uso wake, na kukunjamana taya zake”([92]), Imamu An-Nawawiy aliongeza: “Na kusinyaa korodani zake huku ngozi ikining’inia chini, likidhihiri hili, basi atajulikana kuwa amekufa”([93]).

Kwa hiyo, kifo cha kisharia hupatikana kwa roho kuuacha mwili, na kwa kuonekana kwa dalili za kifo ambazo zinajulikana kwazo kuthibiti kifo, na haitoshi shaka au dhana.

Ama uhakika wa kitaalamu wa kifo cha ubongo: ni kukoma moja kwa moja kwa kazi za ubongo.

Na wataalamu wa matibabu wametofautiana kati yao wenyewe katika kuanisha kukoma huku, kwa kuzingatia rai mbili:

Rai ya kwanza: Kifo cha ubongo ni kukoma kwa kazi zote za ubongo, kukoma moja kwa moja. hii ni rai ya wasomi wa Marekani.

Rai ya pili: Kifo cha ubongo ni kukoma kwa utendaji wa shina la ubongo pekee, kukoma moja kwa moja. Hii ni rai ya wasomi ya Uingereza.

Hivyo basi, ni wazi kwamba rai ya kidaktari haijaafikiana juu ya kauli moja katika jambo hili, hatuwezi kukata kauli kisharia kwamba kifo cha ubongo ndio mwisho wa maisha ya binadamu au la, au kumzingati mtu aliyekufa ubongo kuwa amekufa au la.

Kwa ufupi: Suala la kifo cha ubongo ni suala lenye utata miongoni mwa madaktari, na lau kama wangekubaliana, watu wa Sharia wasingetofautiana, na rai hizi mbili za kidaktari zinabakia kuwa sawa, na hadi sasa hakuna chochote kinachotufanya tupendelee upande mmoja juu ya mwingine.

Kwa upande wa vitendo, ni busara zaidi kuzingatia asili, ambayo ni kwamba roho inabaki katika mwili; Kwa sababu yakini haiondolewi kwa shaka, na yakini katika hali hii yenye utata ni uhai wa mgonjwa, na shaka ni kuwa amekufa kwa sababu ubongo wake umekufa, au yuhai kwa sababu moyo wake unadunda?

Sura ya nne

Masuala katika hukumu ya kurudisha viungo vilivyokatwa kwa Hadi au kisasi

Kama mkono wa mtu ukikatwa iwe kwa Hadi au kisasa, je, kunajuzu kuurudisha?

Kabla ya kuanza katika masuala haya kwa upande wa kisharia, ni lazima kuweka wazi kwa upande wa kitiba:

Kazi hii inafanyika kwa kuandaa sehemu mbili ambazo zinapaswa kuunganishwa - sehemu ya kiungo kilichokatwa na eneo lake - kisha daktari wa upasuaji huunganisha mishipa ya damu na kushona mishipa na misuli.

Sio viungo vyote vilivyokatwa vinaweza kurejeshwa mahali pao, lakini hii ni maalumu kwa viungo fulani na masharti ambayo lazima yatimizwe katika kiungo hicho kilichokatwa, muhimu zaidi ni: kwamba kisiharibike kwa namna kinashindikana kurejeshwa, na kutokuwa na muda mrefu; Kwa sababu hii inazuia mafanikio ya mchakato wa kuunga, ambao unahitaji sehemu kuwa mbichi na kutokuwa na muda mrefu na tukio la kukatwa.

Kinachodhihiri - Mwenyezi Mungu anajua zani - ni kauli inayokataza kurejeshwa kwa kiungo kilichokatwa kwa Hadi au kisasi; kwa haya yafuatayo:

Kwanza: Kauli ya Mwenyezi Mungu kuhusu wazinifu: (Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini)[An-Nuur, 2], hii imejulisha uharamu wa kuwahurumia wenye kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kufanya kosa la wizi au kumdhuru mwenzake kwa kukata kiungo cha mwenye kufanya aliyoharamisha Mwenyezi Mungu na mipaka yake, hakuna kuwahurumia kwa kurudisha kiungo kilichokatwa baada ya kupitishwa Hadi.

Pili: kwamba Mwenyezi Mungu Anasema: (Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima) [Al-Maidah, 38], hii imejulisha kwamba malipo hayatimii ila kwa kukata, na adhabu haitimii isipokuwa kwa kuona mkono uliokatwa. Vilevile hukumu hii ya kukata inawajibisha kuutenganisha na mwili milele, na kuurudisha ni kwenda kinyume na hukumu ya kisharia, hivyo hakujuzu kuurudisha.

Tatu: Kwamba Mwenyezi Mungu Amesema: (Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa) [An-Nahl, 126], na Amesema Mwenyezi Mungu: (Na kwa majaraha kisasi) [Al-Maidah, 45], na kurudisha kiungo kilichokatwa kwa kisasi kunaondoa mfanano([94]).

Nne: Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abii hurayra R.A.: kwamba Mtume S.A.W. aliletewa mwizi ameiba nguo, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika huyu mtu ameiba, akasema Mtume S.A.W.: Sidhani kama ameiba, yule mwizi akasema, ndiyo (nimeiba) ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume S.A.W. akasema: Mchukueni mkateni mkono wake kisha ichomeni moto sehemu iliyokatwa (ili kusimamisha kuvuja damu) kisha mleteni, akakatwa kisha akaletwa, akasema: tubia kwa Mwenyezi Mungu, akasema: Nimetubu kwa Mwenyezi Mungu, akasema: Mwenyezi Mungu amekubali toba yako([95]).

Kuchoma moto sehemu iliyokatwa ili kukata damu ili njia ya damu izibe, kwa sababu huwenda damu ikatoka na kusababisha uharibifu, na dhahiri katika Hadithi hii inaelezea ulazima wa kuchoma; kuwa ni amri isiyoweza kuwa na maana nyingine isiyokuwa hiyo ambayo ni wajibu.

Hadithi hii inatoa dalili ya uharamu wa kurudisha kiganja sehemu yake, na Sharia imeamrisha kukata na kuamrisha kuchoma kuwa ni tiba yake, na haikutaja kingine, na hili lipo katika sehemu ya kubainisha hukumu na kinacholazimu, ikajulisha kuharamisha kurudisha kiganja kilichokatwa; kwa sababu kanuni iliyopitishwa katika Usuul: Kwamba kunyamaza sehemu inayohitaji maelezo inajulisha kutosheka([96]).

Tano: Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abdurrahman bin Muhayriz, amesema: Tulimuuliza Fudhalab bin Ubeyd kuhusu kuufunga mkono katika shingo ya mwizi, je, ni Sunna? Akasema: Mtume aliletewa mwizi akakatwa mkono wake, kisha akaamrisha ukafungwa shingoni kwake([97]).

Kuufunga mkono shingoni mwa mwizi ni kuhakikisha adhabu ambayo ameitaja Mwenyezi Mungu katika Aya ya wizi, inazingatiwa kuwa ni katika kutimiza adhabu, na kurudisha kiganja sehemu yake kunaondosha kutimiza adhabu inayotakiwa kisharia, hakujuzu kufanya hilo([98]).

Sita: Hadithi ya mwanamke wa kabila la Al-Makhzoumy ambaye aliiba na Maquraysh wakabeba suala lake, wakamuombea kwa Mtume S.A.W., hakukubali uombezi wao na akaamrisha kukatwa mkono wake([99]).

Hadithi inatoa dalili kwamba: Kulikuwa kunawezekana kukata mkono wake, kisha akamuomba Mwenyezi Mungu akamrudishia mkono wake, akakusanya kati ya kusimamisha Hadi na kutekeleza matakwa ya Maquraysh, lakini hakufanya hivyo, hilo likajulisha kwamba hakuna njia ya kurudisha kiganja kilichokatwa, pamoja na kwamba Mtume S.A.W. alirudisha jicho la Qatada baada ya kutoka katika jihadi, likawa jicho zuri zaidi.

Siri katika hili ni kwamba, mwenye kukatika na kiungo kwa sababu isiyoharamu, kunajuzu kwake kukirudisha kwa matibabu, na mwenye kukatika kiungo kwa Hadi, hakujuzu kukirudisha([100]).

Saba: Kauli ya kurudisha kiungo kilichokatwa kwa Hadi au kisasi inaondosha hekima ya kuwajibisha hadi au kisasi, nayo ni kukemea, kusalia sehemu iliyokatwa kiungo, kunakumbusha mtu adhabu aliyopata, hivyo atahofia kurudia, kinyume na kama atajua kuwa kiungo kilichokatwa kitarejeswa kama kilivyokuwa, hili linamfanya adaharau adhabu na kumhamasisha yeye na wenzake kufanya makosa. na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi. 

Mwisho

Mwisho wa utafiti huu tunafupisha matokeo yafuatayo:

Kunajuzu kuhamisha kiungo kutoka katika mwili wa mwanadamu aliye hai kwenda sehemu nyingine  katika mwili wa mwanadamu huyo huyo katika dharura na haja, ama kwa urembo hukumu yake inatofautiana kutokana na njia zake.

Hakujuzu kuhamisha kiungo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliye hai kwenda kwa mwanadamu mwingine.

Hakujuzu kuhamisha kiungo kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliye hai kwenda kwa mwanadamu mwingine kwa biashara.

Kunajuzu kuhamisha viungo visivyokuwa kimoja kimoja kutoka katika mwili wa mwanadamu aliye hai kwenda kwa mwanadamu mwingine kwa kutoa bure kwa vidhibiti.

Kunajuzu kuhamisha viungo vya maiti na kuvipandikiza katika mwili wa mwanadamu aliye hai kwa vidhibiti.

Hakujuzu kuhamisha viungo vya uzazi ambavyo vinanasababisha kuchanganya koo.

Kunajuzu kunufaika na kujitibu kwa viungo vya wanyama waliotwahara, ni wale wanaoliwa nyama zao, na hakujuzu kwa wanyama ambao ni najisi, na mfu wa mnyama anayeliwa nyama yake au asieliwa.

Kunajuzu kuhamisha damu kwa njia ya kujitolea, hakujuzu kuuza.

Kunajuzu kupata vimelea vya shina na kunufaika navyo kwa lengo la matibabu au kufanya tafiti ya kisayansi iliyohalali, ikiwa haina madhara kwa anayechukuliwa vimelea hivyo, na hakujuzu kuchukua kwa njia ya haramu.

Kifo cha kisharia hakithibiti isipkuwa kwa roho kutengena na mwili, na kwa kudhihri kwa alama za kifo ambazo huthibithi kifo, na haitoshi shaka au dhana. Kuna sharti kwa anayehamishwa kiungo kuthibiti kifo chake kisharia kwa roho kutengana na mwili, ama kuhamisha kwa mtu aliyekufa ubongo ni haramu kwa sababu hilo ni kama kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuuwawa isipokuwa kwa haki.

Hakujuzu kurudisha viungo vilivyokatwa kwa Hadi au Kisasi.

Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Na sifa njema ni zake ambaye kwa Neema Zake hutimia mambo mema.

Muandishi:

Mustafa Abdulkarim Murad (Mtafiti sehemu ya tafiti za Kisharia).

24/4/2007 A.D

Marekebisho yamefanyika kwa kufuata maelekezo ya Prof. Al-Muhakkam 5/2/2009 A.D

Rejea makala halisi:

Ahmad Mamdouh Saad (Mkuu wa tafiti za kisharia).

Imesomwa na kupitishwa na:

Prof. Saad Al-Deen Al-Hilaly (mwalimu Chuo kikuu cha Al-Azhar).

 

([1]) Ulazima unafungamana na moja ya makusudio matano ya kisheria: nayo ni: Dini, Nafsi, Akili, heshima na mali. Haja ipo katika kupanua na kuondoa usumbufu na uzito. Na mapenzi ni: kila lilitoka katika ulazima au haja.

([2]) “Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 335.

([3]) Tazama kitabu cha  Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa ” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 335: 336.

([4]) Al-Ashbaahwa Al-nadhaair cha Alsuyouty.

([5]) Sahih Albukhay (20114).

([6]) AlIjmaa cha Ibnu Almundhir

([7]) Almabsout cha AlSaekhy 15/125

([8]) Mawahib Aljalil Sharhi Khalil cha Alhattab 4/265, Almajmou Sharh Almadh’hab Cha Alnawawiy 9/304, Kashaf Alqanaa An Mutnil Iqnaa cha Bahouty 3/154.

([9]) Almabsout cha Alsarkhy 26/63,/10/218

([10]) Miongoni mwao- waliosimama katika hilo- Dkt. Muhammad Naeem Yassin- Mwalimu kitivo cha Sharia chuo kikuu cha Jordan na mjumbe wa jopo la Fiqhi la kimataifa- katika tafiti yenye kichwa: “ Kuuza viungo vya mwanadamu” miongoni mwa tafiti za kongamano la tatu la Shirika la Kiislamu la sayansi za kitabibu ambalo limefanyika chini ya kichwa: Mtazao wa kiislamu baadhi ya shughuli za kitabibu.

([11]) Masuala ya kuhamisha umiliki ni maarufu na yamethibiti kisheria kwa wanazuoni wa Fiqhi, wanazuoni wa Kishafii wameyaelezea katika matawi yao, kama ilivyokuja katika kauli yao katika kujuzu kuchukua mswaki uliokatwa katika eneo la haram na kutojuzu kuuza, lakini kunajuzu kuchukua badala yake katika njia ya kuondosha umiliki. Tazama suala hili katika Hashiya Al-shabramalsy alaa nihayat Almuhtaj ilaa alminhaj cha Al-Ramly 3/355,356, na Hashiya Alsharawany alaa Tuhfatul Muhtaj fii sharh Alminhaj cha Ibnul Hajar Alhaythamy 4/194.

([12]) Al-Ashbaahwa Al-nadhaair cha Alsuyouty

([13]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, Uk. 372: 373.

([14]) Miongoni mwa fatwa ambazo zimetolewa na jopo la fatwa la baraza la kuu kiislamu Algeria tarehe 6 mfungo mosi 1392 Hijry (Aprili 20 1972 A.D)  kuhusu “kuhamisha damu na kupandikiza viungo”. Jarida la Tafiti za Kiislamu- hutolewa na uongozi wa idara kuu za tafiti za Kisayansi na Fat’wa na Daawa na uongofu- Riyadh. Toleo nambari 22 uk 47.

([15]) Ahkam Als-shar’iya li Aamal  Al-tibbiya” cha Dkt. Ahmad Sharafudeen, uk. 135, Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 376.

([16]) Al-Ashbah wa Annadhwaair cha Al-souyouty uk 83, 84.

([17]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 376: 377.

([18]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 374.

([19]) Durarl Al-Ahkam 1/40,41.

([20]) Al-Ashbah wa Annadhwaair cha Al-souyouty uk 87.

([21]) Makala: Kuhamisha viungo vya mwanamu ya Shekhe Jad Al-Haqq- ili na jarida la Al-Azhar sehemu ya kumi na tisa mwaka 55 toleo la Ramadahani mwaka 1404 Hijriya sawa na Juni 1983, Shafaa Al-Tabarih cha Yakuoby uk 21, Tafiti: “kuhamisha damu na viungo au sehemu katika kiungo kutoka kwa mwanadamu kwenda kwa mwingine”. Jopo la kudumu la tafiti za kisayansi na Fat’wa- iliyochapishwa na jarida la tafiti za Kiislamu-. Toleo nambari 22 uk 41.

([22]) Al-Hashiya Ibnu Abideen (Radd Al-muhtar All Aldaar Al-Mukhtar) 2/238,239.

([23]) Manh Al-Jalili Sharh Mukhtasar Khalil 1/530:532

([24]) Al-Tajreed linafilabeed 1/498,499.

([25]) Futuhata Alwahab bisharh manhaj Al-tullab 2/212

([26]) Kashaf Al-Qannaa an Matn Al-Iqnaa 2/145, 146.

([27]) Ahkam Eljeraaha” cha Dkt. Alshanqity, uk. 375: 374.

([28]) Amajmou /946,47.

([29]) Ahkam Eljeraaha” cha Dkt. Alshanqity, uk. 379: 381.

([30]) Fatawaa Al-Islamiya  kutoka ofisi ya Mufti wa Misri Juzuu ya kumi uk 3702 na kuendelea tarehe 5/12/1979A.D.

([31]) Ni kauli ya Shekhe Al-Sharawy, ameandika hekima ya kuhusu hekima ya suala hili na msimamo wake, ikiwemo makala ya yenye kichwa: “Mwanadamu hamiliki mwili wake, vipi ajitolee ajitolee sehemu ya mwili wake au auze?” ilichapishwa katika jarida la Al-Liwaa Al-Islamiy toleo namba nambari (226) Alhamisi tarehe 27 mfungo tisa 1407 Hijry sawa na 26 Februari 1987 A.D., na jarida la Al-Aalam la kila wiki  toleo nambari (469) Jumamosi 14  Shaban 1413 Hijry sawa na tarehe 6 Februari 1987 A.D. na Sheikh Abdallah bin Al-Sedeeqk Al-Ghamary. Na rai yake katika suala hili katika makala aliyoita: “Taarif Ahlil Islama bi annanaqli Al-udhwu haram” na Shekhe Al-Sanbahly. Na neno lake katika tungo yake: “Qadhaya Fiqhiya Muaasara”. Na Shekhe Al-Saqaf ametunga makala katika masuala haya, yenye kichwa: “ Al-Imtinaa wal-Istiqsaa liadillat tahreem naqli Al-Aadhaa”, na Dkt. Abdussalaam Abdurraheem AlSukkary- Mwalimu wa kitivo cha Sharia na sheria chuo kikuu cha Al-Azhar, na kauli yake katika kitabu chake: “Naqli waziraat Al-Aadhaa Al-Aadamy min mandhour Al-Islamiy”, na Dkt. Hassan Ally Al-Shadhly- Mwalimu na mkuu wa kitivo cha Shariana sheria chuo kikuu cha Al-Azhar- na rai yake katika tafiti yake: “ Intifaa Al-Insaan biaadhaa jism aakhar hayyan au mayyitan” Nayo ni katika tafiti za jumuia ya Fiqhi za Kiislamu.

([32])  Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 358: 359.

([33]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity uk. 381: 382.

 

([34]) Taarif Ahlul Islam bianna naqli Al-udhuw Haram  uk 14.

([35]) Buhouh fii fiq’hi Al-muaaasar cha Sheykh Hssan Al-Jawahiry 2/341.

([36]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity. Uk. 359: 360.

([37]) Sahih Muslim (116).

([38]) Taarif Ahlul Islam bianna naqli Al-udhuw Haram  uk 20.

([39]) Sahihi Muslim(2122)

([40]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 361.

([41]) Taarif Ahlul Islam bianna naqli Al-udhuw Haram  uk 15,16.

([42]) Sahih Muslim (1731).

([43]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 361: 362.

([44]) Bouhouth fii Fiqhi Al-Muaasar cha Jawahiry.

([45]) Sunan Abou Daouwd (3207), Sunan Ibnu Majah (1616), Musnad Ahmad (105/6), Sunan Ad-Drqutniy (188/3).

([46]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 362.

([47]) Sahih Muslim (971).

([48]) Taaf Ahlul Islam bianna Naqlu Al-Udhwu Haram, uk. 18.

([49]) Alfatawa Al-Islamiya kutoka ofisi ya Mufti wa Misri juzuu ya kumi, uk. 3702 na kuendelea, katika Fatwa za Shekhe Jad Al-Haq Ally Jad Al-Haq tarehe 5/12/1979. Albayan fii taarif asbab al-Hadith Al-Sharif 3/64 nukuu.

([50]) Sunan Ibnu Majah (2341), Musnad Ahmad (313/1).

([51]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 362: 363, Hadithi ni Sahih Bukhary (1654).

([52]) Bouhouth fii Fiqhi Al-Muaasir cha Sheykh Hassan Al-Jawhary 338/2, 339.

([53]) Sahih Muslim (9997).

([54]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 363.

([55]) Angalia Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 362: 363.  Taaf Ahlul Islam bianna Naqlu Al-Udhwu Haram  cha Shekhe Al-Maghmary, uk. 4

([56]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 364. Taaf Ahlul Islam bianna Naqlu Al-Udhwu Haram  cha Shekhe Al-Maghmary, uk. 4,5,12,13.

([57]) Alfatawa Al-Islamiya kutoka ofisi ya Mufti wa Misri juzuu ya kumi, uk. 3702 na kuendelea, katika Fatwa za Shekhe Jad Al-Haq Ally Jad Al-Haq tarehe 5/12/1979

([58]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 364.

([59]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 364.

([60]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 365.

([61]) Kanuni katika Al-Ashbah wa Nadhair cha As-Suyuty, uk. 469, na Al-Amanthour katika kanuni za kifiqhi cha Azakashy 138/3.

([62]) Ahkama Al-Jerah Al-Tibbiya cha Al-Shanqity, uk. 365.

([63])  Al-Iqnaa fii hili Alfaadh abou Shoujaa cha Khatib Al-Shirbiny.

([64]) Dkt. Al-Sukary amezitaja katika kitabu chake: Naqli waziraat AAdhaa Al-Aadamiy uk124:131 na Sheykh Al-Sunbulhaly katika kitabu chake: Qadhaayaa Fiqhiya Al-Muaasara, uk. 62: 63

([65]) Hashiyat Ibnu Abdeen 338/6

([66]) Al-Taaj wal-Ikleel, 4/352,353.

([67]) Al-Mugny, 6/164.

([68]) Hadithi hii katika Sunan Ibnu Majah (3314)

([69]) Kashaf Al-Iqnaa, 6/189.

([70]) Kashaf Al-Iqnaa, 6/198,199.

([71]) Kongamano la: Mtazamo wa Kiislamu katika kupandikiza baadhi ya viungo vya mwanadamu. Lililoandaliwa na shirika la Kiislamu la sayansi ya matibabu Kuweit.

([72]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa ” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 339.

([73]) Badaaii Alsnaaii fii tartiib Al-Sharaaii, 5/132.

([74]) Hashiya Al-Dusouqy Alaa Sharhi Al-kabeer, 1/63.

([75]) Al-Majmouu An-Nawawy, 3/145,146.

([76]) Al-Mughny, 2/211.

([77]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa ” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 402.

([78]) Hashiya Ibnu Abdeen 1/330.

([79])  Kashafat al-qanaa an Matni Al-Iqnaa, 1/292.

([80]) Al-Jaamii Al-Ahkaam Al-Qur’aan.

([81]) Al-Majmou Sharh Al-Madh’hab cha An-Nawawy, 2/576.

([82]) Rejea katika Marejeo yaliyotangulia, na hadithi hii ameipokea At-Tirmidhy (1961) na Ibnu Majah (3427) na At-Tirmidhy amaesema ni Hadithi Hassan Sahih.

([83]) Al-Musannif Abdirazaq, 9/256.

([84]) Radd Al-Muhtar Alaa Al-daar Al-Mukhtar, 5/228, 6/389.

([85]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa ” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk.583.

([86]) Al-Ijmaa, uk. 90.

([87]) Sahih Al-Bukhary (1980).

([88]) Fathul-Bary, 4/427.

([89]) Sunan Abi Dawoud (3488).

([90]) Al-Majmou fii sharhi Al-madh’hab, 9/273, 275, 284.

([91]) Mughny Al-Muhtaj, 3/449, Angalia: Rawdha Al-Talibin, 5/194: 195.

([92]) Al-Mughny, 2/1495.

([93]) Al-Majmou, 5/110.

([94]) Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa ” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 416: 417.

([95]) Al-Mustadrak Alaa Sahihayn cha Hakim, 4/422.

([96])  Taaf Ahlul Islam bianna Naqlu Al-Udhwu Haram, uk. 25: 26.

([97]) Suna Abuu Dawoud (11447) Sunan At-Timidhy (1447, Sunan Annsaaiy (4983).

([98]) Taaf Ahlul Islam bianna Naqlu Al-Udhwu Haram uk,26, Ahkam Eljeraaha Al-tibbiya wal Aathaar Almurattaba Alayhaa ” cha Dkt. Muhammad bin Almukhtar Alshanqity, uk. 418.

([99]) Hadithi hii ni Mutafaqun Alayhi, Sahihi Al-Bukhary (3288), Sahih Muslim (1688).

([100]) Taaf Ahlul Islam bianna Naqlu Al-Udhwu Haram, uk. 26: 27.

Share this:

Related Fatwas