Marehemu kusikia wanaowatembelea makaburini, kuwasalimia na kusikia uwepo wao
Question
Je, Marehemu wanawasikia wanaowatembelea?
Answer
Inajulikana kwamba mwanadamu akifa, basi kifo chake si mwisho wa uwepo wake au hatakuwa na uhai tena, bali ni kuhama kutoka katika uhai kwenda mwingine, kwa hiyo, ingawa kifo na kuzikwa mwanadamu huhisi yanayojiri karibu naye, huhisi wanaomtembelea na kuitika salamu anaposalimiwa, hayo kwa mujibu wa hadithi kadhaa zilizothibitishwa kutoka katika Mtume (S.A.W.); kama vile hadithi ya kuonyesha amali za waislamu juu ya Mtume (S.A.W.) na kuwa anatuombea maghufirah katika hadithi: “Uhai wangu ni heri kwenu, mnafanya makosa nikawafariki, na kifo changu kwenu ni bora ambapo amali zenu naziona, basi nikiona heri namshukuru Mwenyezi Mungu, na nikiona shari nawaombeni maghufirah wa Mwenyezi Mungu” imesimuliwa na Al-Bazzar katika kitabu chake cha “Musnad”, ikaungwa mkono na wengi wa wahifadhi hadithi wakiwemo Imamu An-Nawawy, Al-Hafidh Bin Hajar, Al-Hafidh As-Syuty na wengineo.
Pia, hukumu hii husisitizwa na iliyokuja katika sheria kuhusu hukumu ya kumlakini Marehemu (kumsomesha Shahada mbili wakati wa kukaribia kufa), ambapo asingalisikia wengine wasingalimlakini kwa ajili ya afe akikiri shahada mbili.