Umrah za Mtume (S.A.W.)
Question
Je, ni ngapi idadi ya umrah za Mtume (S.A.W.)?
Answer
Mtume (S.A.W.) alifanya ibada ya umrah mara nne; kwa dalili iliyosimuliwa kutoka kwa Anas (R.A.) kwamba “Mtume (S.A.W.) alifanya ibada ya Umrah mara nne; zote zilikuwa katika mwezi wa Dhul-Qiadah isipokuwa ile Umrah iliyokuwa ikiambatana na Hijja yake ya pekee, na kwamba Mtume alikwenda Umrah kutoka Hudaybiyah, au katika wakati wa mkataba wa Hudaybiyah mwezi wa Dhul-Qiadah, Umrah katika mwaka uliofuata mwezi huu huu wa Dhul-Qiadah, Umrah kutoka Gu’aranah alipoyagawa mavuno ya vita ya Hunain mwezi wa Dhul-Qiadah, na Umrah ya mwisho ilikuwa pamoja na Hijja yake” Imesimuliwa na Muslim.