Sifa maalumu za Mtume (S.A.W.)
Question
Je, makundi ya kigaidi wanaonaje sifa na fadhila alizopewa Mtume (S.A.W.) na Mwenyezi Mungu?
Answer
Sifa maalumu na fadhila za Mtume (S.A.W.) na Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa dhana ambazo zinathibitisha tofauti kati ya fikra sahihi za Waislamu walioongoka na fikra potofu za wenye msimamo mkali, ambapo kuelewa dhana hii huchangia kuainisha hukumu kadhaa, kwa hiyo, kutoelewa na kutotambua sifa maalumu za Mtume (S.A.W.) kumesababisha wenye fikra potofu kuwahukumu baadhi ya waumini kuwa ni makafairi kwa kudai kuwa wanaomba njia ya kumfikia Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume (S.A.W.) katika dua zao, hivyo kuhalalisha kupigana nao, mfano wa hayo, baadhi ya watu wema na mawalii ambao baadhi ya Waislamu wanadhani kuwa wana sifa maalumu na fadhila za pekee, hivyo wanawatembelea na kuomba baraka na ridhaa za Mwenyezi Mungu kwa kujikurubisha nao. Kwa hakika kutoelewa haya yote kunapelekea kuwahukumu Waislamu wanaotekeleza ziara hizo kuhukumiwa ukafiri na kupigana nao pasipo na haki, kwa hiyo kutambua sifa maalumu za Mtume (S.A.W.) ni wajibu hasa kwa mtoaji Fatwa ambaye anatakiwa kupambanua kati ya mambo yaliyopewa Mtume pekee na sifa na fadhila za umma kwa ujumla, kwani sifa hasa za Mtume hazifai kuwa chanzo cha kutunga sharia.
La msingi katika matendo ya Mtume (S.A.W.) kuwa yanawafaa umma wote na yanaweza kutambulikana katika sharia bila ya kuacha chochote isipokuwa kwa dalili sahihi, kwani matini za sharia zimesisitiza kuwahimiza Waislamu kumfuata Mtume katika hali zake zote.
Na miongoni mwa Aya za Qur`ani Takatifu inayoeleza hayo kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana} [Al-Ahzaab: 21]