Kuipenda familia ya Mtume na kuones...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuipenda familia ya Mtume na kuonesha fadhila zake

Question

Ni vipi Sharia ilihimiza mapenzi kwa familia ya Mtume na fadhila zake ni nini?

Answer

Sharia tukufu ilikuja na amri ya kuipenda familia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi katika kujikurubisha” [ASh-Shura: 23], na imepokelewa kwa usahihi kutoka kwa Ibn Abbas, (R.A), katika kuifasiri Aya hii, kama alivyosimulia Imamu Al-Bukhari katika “Sahihi” yake kwamba alisema: “Hapakuwa na ukoo wa Maquraishi isipokuwa ana undugu nao, basi akasema: Isipokuwa nyinyi mdumishe ujamaa uliopo baina yangu na nyinyi” Huu ni pendekezo la undugu wake Mtume, (S.A.W), hali ambayo Mwenyezi Mungu amemuamuru awafikishie watu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) ametuamrisha kuwapenda watu wa nyumbani mwake na kushikamana nao, na akatuusia – amani iwe juu yao – katika Hadithi zake nyingi tukufu, zikiwemo zilizopokelewa kutoka kwa Abdullah bin Abbas, (R.A), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, (S.A.W) amesema: “Mpendeni Mwenyezi Mungu kwa vile anavyokupeni riziki na nipendeni mimi kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na wapendeni Ahlil-bayti wangu kwa mapenzi yangu.” Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi.

Share this:

Related Fatwas