Taratibu ya Swala ya Jeneza.
Question
Ipi taratibu ya Swala ya Jeneza ikiwa wanaoswaliwa ni wanaume na wanawake pamoja na watoto wadogo?
Answer
Ikiwa Swala ya maiti ni mkusanyiko kwa kuwepo wanaume au wanawake au watoto wadoto hutangulizwa mbora wao, ima wawekwe nyuma ya wengine na wanaanza watu wazima na wenye nafasi, au wanawekwa baadhi yao nyuma ya baadhi ya wengine, au wanaweza kuwekwa safu moja, na Imamu anasimama kati kati yao na kuwaswalia, na hufanyika kwa wanawake kama inavyofanyika kwa wanaume.
Wakiwa ni watoto wadogo wa kiume na wakike basi watoto wa kiume ndio wanawekwa karibu na Imamu na wa kike wanawekwa nyuma yao wakifuata Kibla.
Ikiwa Swala ya Jeneza imekusanya wanawake na wanaume basi maelezo yaliyofikiwa na Madhehebu za Kifiqhi na kupokewa na watangulizi wengi miongoni mwa waja wema na Jamhuri ya Wanachuoni ni kuwa hutangulizwa wanaume kwa upande wa Imamu na wanawake wanafuata baada ya wanaume kwa upande wa Kibla, ikiwa wamekusanywa na maiti za watoto wadogo watawekwa nyuma ya maiti za wanaume kisha maiti za wanawake kwa upande wa Kibla.