Kutengeneza michezo ya watoto.
Question
Ipi hukumu ya kutengeneza wanyama na michezo ya watoto?
Answer
Kwa vile michezo hii iliyotajwa haipelekei kwenye ufasiki na kufanya yaliyoharamu, na kutokuwa na dhana za ibada, basi hakuna haramu Kisharia, kwani imethibiti kutoka kwa Mama wa Waumini Bibi Aisha R.A kuwa Mtume S.A.W alimuoa akiwa na mchezo wake.