Ulinganio kabla ya adhana ya Swala ya alfajiri kwa nusu saa.
Question
Ipi hukumu ya Adhana kabla ya adhana ya Swala ya Alfajiri kwa nusu saa?
Answer
Hadithi imepokewa na Maimamu wawili – Bukhary na Muslimu katika Sahihi zao, ni Hadithi kutoka kwa Abdillah Ibn Omar R.A na Mama wa Waumini Bibi Aisha R.A kutoka kwa Mtume S.A.W amesema:
إِنَّ بِلالًا يُؤَذِّنُ بِلَيْلٍ؛ فَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يُؤَذِّنَ ابْنُ أُمِّ مَكْتُومٍ.
“Hakika Bilal huadhini usiku, basi kuleni na kunyweni mpaka atakapoadhini Ibn Ummi Maktuum”. Jamhuri ya Wanachuoni kwa Hadithi hii wakachukuwa dalili ya kufaa kusomwa Adhana kabla ya Swala ya Alfajiri ili kuwajulisha watu kukaribia kuingia wakati wake, na Imamu Bukhari jambo hili akaliweka ndani ya sahihi yake kwenye mlango unaosema (Mlango wa Adhana kabla ya Alfajiri), pamoja na hayo inapaswa pia kuchunga hali za watu na waliyoyazoea, kwani katika Uislamu si ruhusa kudhuru wengine wala kujidhuru mwenyewe, na linapaswa jambo hili kulirudisha pande husika na wala sio watu kufanya haraka kutekeleza hatua hii kwa jitihada zao tu.