Kulea mtoto asiyefahamika ukoo.
Question
Ni namna gani Sharia imependekeza katika kulea mtoto asiyefahamika ukoo na zipi thawabu za hilo?
Answer
Familia ikiwa itasimamia malezi ya mtoto yatima ukoo wake unafahamika huyo mtoto hana wasia kwa maana ya mirathi, au kulea mtoto ukoo wake haufahamiki ili kukulia kati ya watu wa familia hiyo, na kupata malezi na familia kumgharamia kama mmoja wa wanafamilia, ikiwa ni kufidia kwa alichopoteza miongoni mwa mazingira ya kifamilia, basi jambo hili linazingatiwa ni jambo kubwa la kheri linalenga kuimarisha mazingira mazuri kwa watoto ambao wamepoteza familia zao, lengo ni kuwalinda kutopotea, na kuwafanya kuwa watu wema ndani ya jamii zao na kuinufaisha.