Kupoteza matumaini kwa masiku na nambari
Question
Ni ipi hukumu ya kutarajia shari wakati wa kuona nambari maalum au kufika siku au mnasaba maalum katika kile kinachoitwa “Kukosa matumaini?”.
Answer
Kukosa matumaini kwa nambari masiku na mengineyo, Sharia imekataza, kwa sababu mambo yanakwenda kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala hakuna muunganiko wa vitu hivi na kheiri anayoipata mwanadamu au shari inayomfika, kilichopitishwa Kisharia ni kukatazwa kuwa na hali ya kukosa matumani kwa ujumla kwa kuzingatia ni kawaida za zama za ujinga, kama lilivyopokewa katazo la Mtume S.A.W la kupoteza matumaini kutokana na baadhi ya matazizo, kama ilivyopokewa katika Sahihi mbili kutoka kwa Abi Huraira R.A kutoka kwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kuambukiza wala mwezi wa mfungo tano wala ndege kuruka usiku”.
Na hekima ya kuzuia huku ni yale yaliyomo kwenye kukosa matumaini ikiwa ni pamoja na dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuondoa umuhimu wa kufanya kazi, kama vile moyo hugawanyika kwa hali ya wasi wasi.
Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi.