Shaka katika kitu kilichowekewa nadhiri
Question
Mtu ameweka nadhiri kisha akawa na shaka na kitu alichoweka nadhiri, basi ipi hukumu?
Answer
Mwenye kuweka nadhiri kisha akawa na shaka au akasahau aina ya alichowekea nadhiri, je ni swala funga kutoa sadaka au visivyokuwa hivyo, basi anapaswa kujitahidi mpaka ashinde dhana yake kisha afanye hicho, ikiwa amefanya jitihada lakini ameshindwa kujua aina ya alichoweka nadhiri atalazimika kafara ya kiapo, kwa sababu shaka katika kilichowekewa nadhiri ni kama kutokitaja, na kwa kushindwa kwake kuainisha aina ya nadhiri anafananishwa na mwenye kuweka nadhiri ya jambo kisha akashindwa.
Mwenyezi Mungu Anajua zaidi.