Aya za upanga (kuruhusu mapigano) n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Aya za upanga (kuruhusu mapigano) na aya za msamaha

Question

Je, Aya za upanga zimezifuta hukumu za Aya za msamaha?

Answer

Aya za upanga (kuruhusu mapigano) hazikufuta Aya za msamaha, Aya za kuruhusu mapigano ni kama kauli yake Mwenyezi Mungu: {basi wauweni washirikina popote mwakutapo} [At-Tawbah: 5], Aya za msamaha ni kama vile kauli yake Mwenyezi Mumgu:{Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili} [Al-A'raaf: 199], kwa hiyo aya za kuruhusu mapigano hutumiwa katika hali za kujitetea pengine aya za msamaha hutumika katika hali zote, hakuna mgongano wowote kati ya Aya za maana mbili, kwa hiyo kusema kwamba Aya za kuruhusu mapigano hazipingani na Aya za msamaha, pia, wataalamu wa elimu ya vyanzo vya Fiqhi waliweka sharti la kutoweza kukusanya dalili mbili, kwa upande wake Mtume (S.A.W.) alitekeleza yaliyomo katika Aya hizo mbili na Aya zinazofanana nazo katika nyakati tofauti, ambapo Mtume (S.A.W.) alikuwa na mkataba wa Al-Hudaybiya na washirikina kutafuta amani katika jamii ya Madinah, baada ya kupigana nao katika vita ya Badr, Uhud na Al-Khandaq lengo la kujitetea, halafu Mtume (S.A.W.) akafungua Makkah baada ya washirikina wa Qureish kuvunja na kukataa mkataba, baadaye akawaachilia huru na kuwasamehe katika Hadithi yake maarufu aliwaambia waende zao huru, wataalamu walikubaliana kuwa agizo la kuanza vita au amani ni la mtawala kulingana na sera zake ambazo hujali maslahi ya umma.

Share this:

Related Fatwas