Swala ya aliyejitenga na safu

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya aliyejitenga na safu

Question

Je inafaa mtu kuswali nyuma ya safu kwa aliyejitenga?

Answer

Wanachuoni wametofautiana kuhusu kufaa mtu kuswali peke yake nyuma ya safu, Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa na Imamu Maliki pamoja na Imamu Shafi wamesema kuwa mwenye kuswali akiwa peke yake nyuma ya safu kutokana na ugumu wa kuingia kwenye safu Swala yake inafaa bila ya kuchukiza, na ikiwa ataswali peke yake akiwa nyuma ya safu pamoja na kuwepo uwezekano wa kuingia kwenye safu Swala yake inafaa pamoja na kuchukiza, na anapata thawabu za Swala ya jamaa kwa hali zote.

Na Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Hambali wamesema kuwa mtu kuswali peke yake nyuma ya safu pindi akiswali katika hali hiyo rakaa moja kamili Swala yake haifai.

Kutokana na hilo: Mtu kuswali peke yake nyuma ya safu ambayo inamwanya Swala yake ni sahihi pamoja na kuchukiza kuswali hivyo, hilo wala halimzuii kupata thawabu za Swala ya jamaa, na inapendeza kwake kuingia kwenye safu au kumstua mtu mwingine aliyopo kwenye safu kwa upole ili arudi nyuma na kutengeneza naye safu. 

Share this:

Related Fatwas