Kutenga fungu maalum la zaka kuwasaidia wenye madeni na kuhudumia jamii
Question
Ni ipi hukumu ya kutenga fungu maalum la zaka kuwasaidia wenye madeni na kuhudumia jamii?
Answer
Kunajuzu kutenga fungu maalum la zaka kuwasaidia wenye madeni na kusaidia kuboresha kuhudumia za kielimu, na kufanya miradi ya uwekezaji na uzalishaji katika mali za zaka kwa sharti ya kuchunga maslahi ya masikini katika kuitekeleza na kuwamilikisha; kuwatosheleza masikini na wenye mafukara katika mavazi, chakula, makazi, maisha, elimu, matibabu na mengineyo katika mambo ya maisha yao kunapasa kuwa kupewa kipaumbele; ili kufikia hekima kuu ya zaka ambayo Mtume S.A.W. ameilezea kwa kauli yake: “inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa kwa masikini wao”.