Swalah ya Al-Fjiri kwa wanaosafiri kabla yake.
Question
Jinsi ya kuswali Swala ya Al-Fjiri kwa wale wanaosafiri kabla yake?
Answer
Muislamu akianza kusafiri kwenda sehemu yake ya kazi kabla ya Adhana ya Al-Fajiri kisha muda wa Swala ya Faradhi ukaanza: Ikiwa anajua kwa ada kuwa atafika anapokwenda na akaweza kuswali, hali ya kutimiza masharti na nguzo za Swala kabla ya jua kuchomoza; basi aicheleweshe mpaka wakati huo. Na ikiwa atajua kuwa hatafikia chochote katika haya mpaka baada ya kuchomoza jua, na haiwezekani kwake kuswali kwa ukamilifu wa masharti na nguzo za usafiri; aiswali hapo kwa kutimiza masharti na nguzo anazoweza kuzifanya, na baada ya hapo inapendeza arudie Swala ikiwa muda wake umebaki, au ailipe ikiwa muda umeisha.